Nafasi Za Mafunzo Ya Ualimu Katika Vyuo Vya Ualimu Vya Serikali Kwa Mwaka Wa Masomo 2019/2020

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi linapenda kuufahamisha umma kuwa wahitimu wa kidato cha nne na sita wenye sifa watume maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2019/2020. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28/11/2019 na Masomo yanatarajia kuanza 30/11/2019.

Waombaji wa mafunzo haya ni wale wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu katika mitihani ya kidato cha NNE (kwa waombaji wa Astashahada – Miaka Miwili) na kidato cha SITA (kwa waombaji wa Stashahada-Miaka miwili). Waombaji watatakiwa kuomba moja kwa moja vyuoni na watasajiliwa kupitia ‘Instititutional Panel’ ya vyuo husika.

Sifa za kujiunga na programumbalimbali za Ualimu kwa Vyuo vya Ualimu ni kama zilivyoainishwa kwenye Kitabucha Mwongozo wa Udahili (AdmissionGuidebook) kilichopo kwenye tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) ambayo ni (www.nacte.go.tz). Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansina Hisabati, Lugha na Biashara, kipaumbele kitatolewa kwa waombaji wa Stashahada (Miaka mitatu)waliofaulu kwa alama ‘C’ katika masomo mawili ya Sayansi/Lugha/Biashara yakufundisha.

Aidha, vyuo vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tarehe 20/11/2019

1 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post