TCRA: EPUKENI KUANDIKA HABARI ZENYE MIHEMKO NA ZENYE MAONI BINAFSI


Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,akizunguza na wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu.


Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claud Gwandu akiwa katika semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na APC na TCRA
Baadhi ya waandishi walioshiriki katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA)

Wakwanza kulia ni makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wahabari mkoani Arusha Musa Juma akiwa pamoja na waandishi wengine waliohudhuria semiana hiyo ya siku moja 
Na.Vero Ignatus,Arusha

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanyakazi zao kwa  kufuata kanuni mpya zilizoongezwa kwenye sheria mpya ya EPOCA, na kuacha kufanya shughuli zao kwa ushabiki ili kusaidia wanachi kupata taarifa zilizofanyiwa kazi na ambazo zipo katika mrengo sahihi.

Akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na   chama cha waandishi wa  habari mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na TCRA kwa wanahabari Mkoani humo, Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu alisema ni vyema kwa Sasa waandishi wa habari katika shughuli zote wanazozifanya za uandishi ziwe zinaendana na sheria kanuni na taratibu zote walizowekewa ili kuepuka kuingia kwenye migogoro ya kisheria na Mamlaka za Serikali.

AlisemaAPC kwa kushirikiana na wadau wengine inaendelea kufanya mazungumzo na Mamlaka za Kiserikali ili kuondoa kajuni na Sheria ambazo zinaonekana kuminya Uhuru wa habari, hivyo wakati mazungumzo yakiendelea ni vyema Kama wanahabari wakafuata Sheria zilizopo kwanza.

Gwandua Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA)na kusema kuwa mwandishi anahitajika kupewa elimu ,na kukumbushwa masuala yanayogusa moja kwa moja ,katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Mtoa mada katika semina hiyo Afisa  Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Rolf Kibaja ,aliwataka wanahabari kuacha mihemko badala yake waandike habari zenye ulinganifu,mizania na kwa ufasaha sambamba na kujiepusha na maoni yao binafsi.

Kibaja aliwakumbusha waandishi kuwa Tume ya uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kutoa matokeo ya uchaguzi ,na siyo wao kujitwika majukumu ambayo siyo ya kwako,alisisitiza endapo kutakuwa na tashwishwi yeyote ni vyema wakapata majibu sahihi kutoka kwa tume yenyewe

Aliwasihi  wanahabari kuzingatia na kufuata kanuni na maadili maudhui mtandaoni ,pamoja na kuhakikisha habari kabla haijapelekwa kwa walaji lazima iwe na usawa pande zote mbili, ili kuleta tija katika jamii bila kusahau kuzingatia kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2020 namba 343.

Kwau wake Makamu mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani Arusha Musa Juma, aliwasilisha mada isemayo usalama wa waandishi kazini na mitandao ya kijamii ,ambapo alisema kuwa mitandao ya kijamii ina faida na hasara zake,  hivyo aliwataka wanahabari  kuacha kuweka taarifa zao muhimu katika mitandao hiyo ,kwani ni rahisi mtu yeyote kuwafuatilia  na hata kudhurika pia

Aliwataka kufahamu kuwa kwa miaka ya sasa ni vigumu sana kuishi bila kutumia intaneti ,kwa namna moja ama nyingine bali intaneti hiyo ina madhara pia ,kwa mfano: kukumbana na taarifa za uongo,kichaka cha uhalifu, hurahisisha udanganyifu wa taaluma,pia ni chanzo cha kusambaa kwa virusi vya kompyuta.

 Musa alisema kuwa mitandao hiyo ikitumika vizuri zipo fursa mbalimbali za kufungua milango mipya ya chombo kingine cha habari,pia imeweza kuwaleta watu wengi kwa karibu zaidi ila tahadhari ni muhimu mno ,haswa kwa waandishi kwani maisha yao yana thamani kubwa kuliko kitu chochote kile ,hivyo ni vyema wakaitumia kwa umakini wa hali ya juu.

Hivyo aliwataka waandishi wa habari kutawala matumizi yao pamoja na kuzingatia kanuni za usalama kwenye mitandao ili wasiathirike .


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post