Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Takukuru, Ramadhani Ndwatah, alisema mwalimu huyo alipokea Sh 100,000 ili kumsaidia kumrudisha kazini mtumishi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.
Ndwatah alisema Februari 28, mwaka huu, saa 11 jioni, mwalimu huyo akiwa ofisini kwake, alipokea fedha za mtego ili aweze kumsaidia mtumishi wake aliyesimamishwa kazi kurudi kazini.
Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa.