Viongozi Wanne Bodi Ya Maji Makilenga Mbaroni Kwa Ubadhilifu

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Jerry Muro akieleza namna Wilaya hiyo inavyosimamia utekelezaji wa Miradi ili wananchi waweze kunufaika.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,Nelson Mafie   akiishukuru serikali

Naibu waziri wa Maji Mhe. Juma  Aweso  akiongea katika kikao cha awali kabla ya kuanza ziara yake
Waliokamatwa kwa tuhuma za kuhujumu mradi maji wakiwa katika kwenye Gari tayari kwakupelekwa Polisi
Na Woinde Shizza ,Arusha

Naibu waziri wa Maji Mhe. Juma  Aweso, ameagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru kuwashikilia na kuwaweka chini ya ulinzi  viongozi wanne wa  bodi ya  Maji MAKILENGA  Halmashauri ya Meru,Wilayani Arumeru kwa kutuhumiwa  za kufanya ubadhirifu kwenye Mradi huo.
Aweso ametoa agizo hilo baada ya kubaini uwepo wa ubadhirifu wa fedha za mradi huo licha ya makusanyo  ya fedha zinazotokana na uchangiaji wa huduma ya maji kufika  kiasi cha milioni tano (5) kila mwezi bodi imebakiwa na kiasi kisichozidi milioni moja na nusu tu.
“Haiwezekani asilimia kubwa ya mradi unatumia vyanzo vya mtiririko matum izi yake kuwa makubwa kiasi cha kumaliza fedha zote za miaka minne”amehoji Aweso.

Waliokamatwa kwa tuhuma za kuhujumu mradi huo ni pamoja na mwenyekiti wa Bodi Godhope Chales,Mhasibu wa Mradi Warialanga Pallangyo,pamoja na fundi bomba wa mradi huyo anayetambulika kwa jina la Kaaya pia Meneja wa Mradi huo Orest Manyanga amewekwa chini ya ulinzi kwa kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa kikao cha Naibu waziri na wajumbe wa bodi ya Makilenga.
Aidha Aweso ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Maji Kiiji cha Kingori wenye thamani  ya Shilingi bilion 1.5 sambamba na kumpongeza mkandarasi kwa utendaji mzuri chini ya usamizi wa Uongozi wa Wilaya hiyo.
Haya yamejiri wakati wa ziara ya Naibu huyo Wilayani Arumeru iliyolenga kutembelea na kukagua Miradi ya Maji ili kuweza kutambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa Miradi ya maji kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza mpaka kufikia 2025 upatikanaji wa maji vijijini kuwa asilimia 85 na mjini 95,

Akiongea na waandishi wa habari  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru,Nelson Mafie ameipongeza Serikali kwa utatuzi wa changamoto za wananchi  ambapo imeunda chombo cha wakala wa maji vijijini na Mjini (RUWASA) na kusema kuwa huu ndio Mwarubaini pekee  wa changamoto za ya maji .

Kwa upande wa Wananchi  wa wilaya hiyi walitumia mda huo
a Woinde Shizza ,Arusha

Kwa upande wa Wananchi  wa wilaya hiyi walitumia mda huo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro  kwa kutumia fedha zake kumgaramia nauli ya Mzee Senyaeli Mbise Maarufu kama  Lemali, ambaye ni fundi mwenye uelewa wa mradi wa Maji MAKILENGA kurudi kuendelea na kazi hiyo baada ya fundi aliyekuwepo kuwa kikwazo kwenye utendaji Wa mradi huo.

"Kwekweli tunamshukuru Rais wetu kwakutuletea kiongozi ambaye anaupendo na wananchi ,anafanya Kazi vyema ya kutatua kero za wananchi na anaejituma na mchapakazi kwani tangu amekuja ameweza kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazotukabili kwekweli mungu amueke pia tumpongeze pia Rais wetu kwa kufanya Kazi vizuri ya kuwajali wananchi maana bila yeye ata viongozi bora tusingewapata kwani vijana wake aliowateuwa wanafanya Kazi nzuri kulingana na Kazi yake "alisema  Charles akyoo
kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro  kwa kutumia fedha zake kumgaramia nauli ya Mzee Senyaeli Mbise Maarufu kama  Lemali, ambaye ni fundi mwenye uelewa wa mradi wa Maji MAKILENGA kurudi kuendelea na kazi hiyo baada ya fundi aliyekuwepo kuwa kikwazo kwenye utendaji Wa mradi huo.

"Kwekweli tunamshukuru Rais wetu kwakutuletea kiongozi ambaye anaupendo na wananchi ,anafanya Kazi vyema ya kutatua kero za wananchi na anaejituma na mchapakazi kwani tangu amekuja ameweza kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazotukabili kwekweli mungu amueke pia tumpongeze pia Rais wetu kwa kufanya Kazi vizuri ya kuwajali wananchi maana bila yeye ata viongozi bora tusingewapata kwani vijana wake aliowateuwa wanafanya Kazi nzuri kulingana na Kazi yake "alisema  Charles akyoo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post