Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Pili katika mbio za mita 10,000 na kupewa medhali ya Fedha.
Mathayo Sombi Mtanzania aliyeshika nafasi ya Piliakimalizia mbio kama anavyoonekana katika mbio za mita 10,000
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Wanariadha
nchini wameshindwa kutamba katika katika mashindano ya riadha ya vyama
vya michezo kwa shule za Sekondari Afika Mashariki (FEASSSA)
yaliyofanyika Jijini Arusha.
Katika
Matokeo ya jumla kwa wanawake na wanaume nchi Kenya iliongoza kwa
kuondoka na jumla ya Medali 18 za Dhahabu, Medali 11 fedha na medali 10
za shaba na kufanya jumla ya medali 39 sawa na pointi 359.
Uganda
ilifuatia mshindi wa pili kwa kukusanya jumla ya Medali 10 za
dhahabu,Medali 14 za fedha na 10 za Shaba na kufanya jumla ya Medali 34
walizonyakua ambazo ni sawa na pointi 334 huku Tanzania ikishika nafasi
ya tatu kwa kuambulia Medali 2 za dhahabu, Medali 5 za fedha na medali 8
za shaba ambazo ni sawa na pointi 209 .
Nchi ya Rwanda ilishika nafasi ya nne kwa kupata jumla ya medali 2 pekee za shaba na Zanzibar haikupata kitu.
Kwa upande wa wanawake walioshoriki riadha mbio tofauti tofauti Kenya ilifanikiwa kunyakua jumla ya medali 7 za dhahabu, medali 5 za fedha, medali 6 za shaba.
Nchi ya Uganda ilifuata kwa wanariadha wake kufanya kweli kwa kujikusanyia jumla medali 6 za dhahabu,medali 8 za Fedha na medali 4 za shaba huku wenyeji Tanzania wakiambilia medali 2 za fedha,2 za fedha na tano za Shava, huku Zanzibar na Rwanda hazikupata kitu.
Kwa upande wa wanaume Kenya ilijikusanyia jumla ya Medali 11 za Fedha, 6 za fedha na 4 za Shaba , Uganda ilifuata kwa kuwa na jumla ya Medali 4 za dhahabu,6 za fedha na 6 za Shaba ,Tanzania haikupata kitu katika dhahabu,ilipata medali 3 za fedha na tatu za Shaba huku Rwanda ikiondoka na medali 2 za Shaba na Zanzibar haikuambulia kitu.
Matokeo
mengine mwanariadha Faith Kipsang kutoka Shule ya St. francis ya
Kenya alichaguliwa kuwa mwanariadha Bora kwa wanawake huku mwanariadha
Layeng Eric Sibryanda kutoka Gombe nchini Uganda aliibuka mwanariadha
bora kwa wanaume.
Kocha wa timu ya Riadha ya Tanzania katika michuano ya FEASSSA Robert Kalyahe alisema ni kweli wanariadha kutoka Kenya wamefanya vizuri kwa kuondoka na medali za kutosha na Tanzania kupata vichache
" Tumepigwa
kwani pia tumeokoteza tu vijana kutoka mashindano ya Umiseta
yaliyofanyika Mtwara na muda wa mafunzo ulikuwa mfupi,hali ya hewa pia
ilituchanganya hapa Arusha lakini yote kwa yote tumejifunza kutoka kwa
wenzetu Kenya na tutajua nini cha kufanya,"alisema Kalyahe.
Alisema Tanzania inapokosea ni kuweka muda mchache inatakiwa kuweka muda mrefu wa maandalizi vijana wachaguliwe mapema tena ikiwezekana wachezaji wawekwe katika shule moja ili kuwa na maandlaizi ya kutosha.
Naye kocha wa riadha na mjumbe wa kamati tendaji ya Riadha Tanzania Yohana Misese alisema katika riadha inasikitisha kwani watanzania wamekuwa wakienda kwenye mashindano na kurudi bila kufanya tathmini wapi wanakosea .
"Tumeona wenzetu wako makini katika maandalizi na timu wameandaa kwa muda mrefu tofauti na sisi tumeandaa kwa wiki mbili hali inayopelekea kuwa na maandalizi yasiyo na Matokeo mazuri," alisema Misese.