Mahakama
ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemuhukumu Nyamasheki Malima (41),
kifungo cha miaka 60 jela, kwa kumkuta na hatia ya kuwavutisha bangi
watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na 13 wa familia moja,
kisha kuwalawiti.
Akisoma
hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Jacob Ndira amesema kuwa Malima
alitenda makosa hayo kati ya Septemba 2017 na Septemba 2018, baadaye
alikamatwa na kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayomkabili,
lakini alikana kufanya kitendo hicho.
Awali,
Baba wa watoto hao, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kubaini hali hiyo kwa
mtoto mmoja wapo akiwa katika hali isiyo ya kawaida, baada ya kumfanyia
uchunguzi na kuwahoji ndipo walimtaja mtuhumiwa ambaye alikuwa
anawafanyia vitendo hivyo.
Hakimu
Ndira, amesema mahakama ilisikiliza maelezo ya ushahidi wa pande zote
mbili na kuridhika bila ya kuacha shaka yeyote huku mshtakiwa akijitetea
mwenyewe.
Kwa
mujibu wa majibu ya vipimo yaliyotolewa na daktari aliyewafanyia vipimo
watoto hao, unaonesha kuwa sehemu za haja kubwa zilikuwa zinaingiliwa
kila wakati baada ya kuwavutisha bangi watoto hao ambao ni wanafunzi wa
shule ya msingi.
Kutokana
na maelezo ya kina ya kitabibu ya daktari, hakimu Ndira amesema
mahakama imejiridhisha watoto walileweshwa bangi na kulawitiwa.
Hakimu
alipo muuliza mshtakiwa kama ana chochote cha kujitetea kwanini
mahakama impunguzie adhabu, yeye alidai hana nguvu za kiume hivyo
asingeweza kufanya kitendo hicho na kuiomba mahakama imsamehe.
Baada
ya utetezi wake Hakimu Ndira alimwambia mtuhumiwa hana namna ya
kupunguziwa adhabu, hivyo atakwenda jela miaka 60 kutokana na makosa
mawili ya kuwavutisha bangi na kulawiti watoto.