IGP Simon Sirro amekabidhiwa bendera na kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika EAPCCO.
Umoja
huo unaundwa na nchi za Burundi, Comoros, Djibouti, DRC, Eritrea,
Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, South Sudan, Sudan, Tanzania na
Uganda.
IGP
wa Sudan Adil Mohamed Ahmed, akikabidhiwa bendera ya Shirikisho la
Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika ili aweze kumkabidhi IGP Sirro,
ishara ya kumwachia kijiti cha uenyekiti wa Shirikisho kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ni miongoni mwa wanaoshuhudia IGP
Sirro akikabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki
Mwa Afrika kutoka kwa IGP wa Sudan (PICHA- Jeshi la Polisi)