IGP SIRRO AWAONYA VIKALI ASKARI POLISI,AHAIDI KUWAFUKUZA KAZI WANAO KWENDA KINYUME NA JESHI HILO.

Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Simon sirro awaonya vikali askari polisi wanao kwenda kinyume na sheria na sera za jeshi hilo kwa kukeuka miiko ya kazi za jeshi la polisi hapa nchini na kuahidi kutowavumilia askari wote wanao kwenda kinyume na jeshi hilo.
IGP Sirro ameyasema hayo jijini Arusha alipo kuwa anakabidhi nyumba 6 za askari polisi katika makao ya askari polisi njiro jijini Hapa nyumba hizo ambazo ni miongoni mwa nyumba 400 za askari polisi zinazo jengwa nchi nzima na zilizinduliwa na  Rais Magufuli Mkoani Geita siku kadhaa zilizo pita. 
Aidha ameeleza kwamba kufuatia vitendo vingine amabavyo haviendani na jeshi hilo hato weza kuvivumili atahakikisha wanafukuzwa kazi akari wote wanao husika na vitendo hivyo na kuchukilia hatua kali za kisheria na kuwataka askari kuacha tamaa zisizo kuwa na tija.

"Ni mpongeze Rais magufuli kwa kujipatia  shilingi Bilioni 3.5 kwaajili ya kununua Helkopta maalum kwa jili ya Jeshi letu la polisi na pia Bilion 10 kwaajili ya kushona sale mpya za askari polisi na mpaka sasa tumeshampata mkandarasi atakae fanya kazi hiyo yabushonaji sale zetu,pia niwapongeze askari wote ambao mnafanya kazi kwa uweledi na kuzingatia umoja na ustawi wa nchi yetu kwa kulinda amani ya raia na mali zao pia hata kupambana na uhalifu kwa kiasi kukubwa mmeiweka nchi yetu mahali pazuri sasa". alisema IGP Sirro.

"Ila pia haya yote tunayo yapata kutoka kwa Rais wetu ni kutokana na kufanya kazi kwa moyo mmoja ma uweledi pia nimpongeze mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jeshi la polisi hapa Arusha maana ametusaidia kwa hatua kubwa sana toka ujenzi wa nyumba za askari zilizo ungua hadi sasa anazidi kutupatia sapoti kubwa sana, Pia RPC naona yupo vizuri na ndiyo maana hata nyie mnafanya kazi kwa weledi kwa kuiga mfajo wake mzuri wa utendaji kazi". aliongeza IGP Sirro.

Kwaupande wake Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana ameeleza kwamba nyumba hizo walizo kabidhiwa askari polisi zinatoa hamasa katika utendaji wa kazi na itachangia kwa kiasi kikubwa askari kuzidi kupenda kazi zao na kuwa karibu na kazi hata pia itapungiza changamoto ya umbali wa makazi kwa askari hao.
 
 
 
IGP Siro amesema mpaka sasa wameshawashikilia askari kadhaa  kwa kesi ya kuwa uzia sale za jeshi hilo askari wenzio kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa jeshi hilo na ni kitendo kinacholeta utengano wa kazi ndani ya jeshi la polisi hapa nchi.



Aidha pia mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza serikali kwa jitihada hizo madhubuti na kuahidi yeye kama Meenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalma mkoa wa Arusha atahakikisha kila mwaka Jeshi la polisi mkoani Arusha linapata nyumba sita za makazi kwa askari hao.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post