Jamii yataka serikali kuwatia mbaroni wazazi wanaotorosha watoto shule kwa ajili ya kazi za ndani mijin

Baadhi ya wazazi na walezi katika Kijiji cha halmashauri ya mji wa Njombe wamesema njia pekee ya kudhibiti mimba mashuleni na tabia za wazazi kutorosha watoto mijini ili kufanya kazi za ndani hatua ambayo inawafanya kugeuka watumwa ni kuanzisha adhabu ya kifungo Cha miezi sita kwa mzazi yeyote atakaebainika kuhusika na uovu huo.

 Image result for Mimba za utotoni


Rai hiyo imetolewa mara baada ya mahafali ya darasa la Saba katika shule msingi yenye kiwango kizuri cha cha kitaaluma Echo primary school ambapo Paul Kivavi wamesema Njombe imekumbwa sana na janga la mimba na watoto kukimbizwa mijiji kufanya kazi Jambo ambalo linakwamisha ndoto za watoto na mipango ya serikali hivyo adhabu ya kifungo jela Cha miezi sita ianze  kutolewa kwa wazazi wanaobainika kuhusika ili kudhibiti matukio hayo .


Wakati wazazi wakitoa msimamo huo wanafunzi ambao wapo kwenye kipindi Cha matazamio ya matokeo ya kujiunga na kidato Cha Kwanza wamesema kwamba licha ya baadhi ya jamii fulani kushinikiza watoto kufanya vizuri katika mitihani na kuamua kuwatorosha mijini lakini pia wazazi wengi wamekuwa wakizembea katika malezi yenye maadili katika kipindi na kusababisha kukengeuka .


Awali mgeni rasmi ambaye meneja wa crdb mkoa wa Njombe akitoa wasaha kwa wazazi na wanafunzi ametaka wazazi kuwapa watoto urithi wa elimu na kutoa ahadi ya kumkatia bima mwanafunzi mmoja wa darasa la pili ambaye ameonekana kukonga nyoyo za hadhara iliyohudhuria mahafali hiyo katika somo la sayansi .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post