KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, BUKOBA YAKUTANISHA ALBINO KUJADILI USALAMA WAO

Katika kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika vizuri bila kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualubino na matukio mengine yanayoweza kuondoa amani katika jamii Ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na chama cha watu wenye ualubino Bukoba (TAS) wameamua kukutana na watendaji wa kata zote za manispaa hiyo hili kujadili namna watakavyoweza kuwalinda hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Bukoba Japheth Musa Kanoni amesema kuwa wamefaulu kukutana tena kwenye kikao na watendaji wa kata zote za manispaa ya Bukoba cha kujadili ulinzi na usalama kwa watu wenye ualubino hasa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

"Kitu ambacho timekifanya kwa watu wenye ualibino wenyewe kwanza kuepuka kufanya shughuli kwenye maeneo hatarishi na kitu kingine kufanya shughuli zao mapema kwa zile ambazo ni muhimu kufanyika maana ualifu mwingi unafanyika katika mazingira ya kificho au gizani lakini pia wasiende mahali  kwa mda mrefu bila kutoa taarifa kwa wana familia ila waweze kuwapatia ulinzi wao wenyewe" Alisema Japheth Kanoni.

Kwa upande wake katibu wa chama cha watu wenye ualubino Manispaa ya Bukoba  Frolensi Felisian amesema kuwa kwa mwenendo uliopo hivi sasa hali ya usalama imeimarika kuanzia ngazi ya wilaya mpaka kwenye mitaa na kusema kuwa wanaimani uchaguzi utafanyika na kuisha salama.

"Niikumbushe jamii kwa wale ambao bado wanaweza kuona alafu wakakaa kimya naomba tuone umuhimu kama askari anavyoona mtu anafanya ualifu stand alafu akamchukulia hatua pale pale ya kumshika na kumpeleka kituoni na katika hili tukifanya kutoa taarifa na kushirikiana kwa pamoja tutaweza kuokoa maisha ya watu wenye ualbino ili na wao waishi kwa amani na waweze kujitokeza kupiga kura muda mwingine kuweza kugombea". Alisema Frolensi Felisian.
 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post