Kundi B imezikutanisha Olympiacos iliyomaliza kwa sare ya 2-2 na Tottenham Hotspurs, huku Bayern München ikiilaza FK Crvena Zvezda goli 3-0.
Na katika kundi C, Dinamo Zagreb imeifurumishia mvua ya magoli 4-0 Atlanta, nayo Shakhtar Donetsk imekubali kichapo cha goli 3-0 toka kwa Manchester City.
Michezo ya mwisho ilikuwa ni kundi D, Atletico Madrid imetoshana nguvu ya goli 2-2 na bibi kizee wa Turin Juventus, nao Lokomotiv Moscow ikiimaliza Bayer Leverkusen kwa goli 2-1.