Mjane alazimika kuishi kwenye kibanda porini kukwepa manyanyaso ya watoto

Mjane Mariam Mnyang'au (55)mkazi wa kijiji cha Mahenge wilaya ya Kilolo mkoani Iringa akiwa katika makazi yake porini baada ya kudai kunyanyaswa na watoto wake baada ya mume wake kufariki (PICHA NA FRANCIS GODWIN

Na Francis Godwin Iringa 

Mwanamke mjane mkazi wa kijiji cha Mahenge wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa Mariam Laurent Mnyang'au (55) amejikuta katika mateso makubwa baada ya manyanyaso anayopata kutoka kwa watoto wake hivyo kulazimika kukimbia nyumba na kwenda kuishi porini mwenyewe kukwepa mateso.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyemtembelea eneo la pori analoishi kwenye kibanda ambacho kimejengwa kwa miti na kuezekwa nyasi eneo  moja pekee ambalo  ametandika mkeka wa kulalia na robo tatu ya kibanda hicho ikiwa wazi. 

Mwanamke huyo alisema kuwa mateso hayo yamekuja baada ya mume wake kufariki  na watoto hao  kuanza kumtesa kwa lugha cha matusi na hata kutishia kumpiga wakitaka kuachiwa mali mbali mbali alizoziacha  marehemu mume wake. 

"Tatizo mume wangu alikuwa  ametuoa wanawake wawili bibi mkubwa yupo na mimi ni bibi mdogo sasa watoto wake ni magaidi sana wamekuwa wakishirikiana nae kuninyanyasa pale nyumbani kweli nilishindwa uvumilivu nikaamua kuja kuishi hapo "alisema 

Alisema zaidi ya miaka 25 amedumu kwenye ndoa na mume hyo ila toka afariki  amekuwa akiishi kwa mateso toka mumewe alipofariki dunia na kuwa pamoja na mali nyingine marehemu alikuwa na nyumba ila mali zote aliziacha na kuondoka na nguo zake pekee kwenda porini hapo kuanza maisha mapya. 

Aidha alisema tatizo  jingine la mateso na kukosa kudai mali ni kitendo cha kutoachwa wosia wowote na kama kungekuwa na wosia basi amgeweza kudai mali zake .

Hata hivyo alisema mwanga wa kuanza kupambana kutafuta ardhi ya kumiliki mwenyewe aliupata baada ya elimu iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la ISICO chini ya mratibu wake Raphael Mtitu hivyo kutokana na elimu ya haki ya wanawake na watoto wa kike kumilikishwa mali kijiji kilikwenda mpimia eneo hilo alilojenga na kwa nguvu yake kajenga kibanda hicho.

"Ninatamani kuwa na nyumba ya kisasa kama wasamaria wema watajitokeza kunisaidia ila kwa sasa uwezo wangu umeishia hapa na sijui kipindi cha mvua hali itakuwaje maana sijaweza funika sehemu yote ya kibanda na kama unavyoona kibanda hakina hata mlango na huku kwetu mara moja moja tembo huwa wanakatisha ila namwachia ulinzi Mungu kwani kwa sasa ana miezi miwili eneo hilo.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mahenge Said Mhina alisema kijiji kimekuwa na utaratibu wa kuwamilikisha Ardhi wanawake na kuwa mwanamke huyo baada ya kufika ofisini kuomba ardhi alipewa eneo hilo ambalo limetengwa kwa ajili ya makazi .

Kuwa wanawake wanaoteseka katika ndoa kwa kutopewa Ardhi kijiji kimeanza kuwapa maeneo ya kujenga na kulima. 

Mratibu wa ICISO Raphael Mtitu alisema toka shirika lake limeanza kutoka elimu vijiji wanawake na watoto wa kike sasa wameanza kupewa haki sawa katika umiliki wa mali na kupongeza kijiji cha Mahenge kwa kutoa Ardhi kwa mjane huyo huyo.

Kwa mawasiliano na mwanamke huyo wasiliana na mwandishi wetu Francis Godwin 0754026299

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post