Msumbiji, Kenya na Tanzania zaanzisha mradi wa kukusanya takwimu za Samaki

Miongoni mwa samaki wanapatikana ukanda wa nchi za Kenya, Tanzania na Msumbiji

Nchi tatu za ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi Tanzania, Kenya na Msumbiji zimeanzisha Mradi wa Ukusanyaji Takwimu za Samaki kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (Fidea) ili kuwa na taarifa za pamoja zitakazosaidia kulinda na kujua hali ya viumbe hao. 

Katika kikao cha pamoja cha kujadili mradi huo, wadau kutoka nchi wanachama wameshiriki kutoa maoni yao kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Ujerumani. 

Takwimu hizo zitakusanywa kwa njia ya kiteknolojia katika timu ya wasimamizi wa nchi zote tatu halafu zitachakatwa na kupata habari zitakazosaidia kufanya uvuvi endelevu. 

Wanachama wameeleza madhara ya kutokuwa na takwimu za samaki ni kuisha kwa rasilimali hizo huku washiriki wakitolea mfano wa Canada Mashariki kuwa wamezuia shughuli za uvuvi kwa miaka 30 kwa uvuvi uliopitiliza bila ya kuwa na kumbukumbu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post