MTALII AFARIKI AKIRUKA ANGANI NA PARACHUTI KUTOKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Justin Kyllo (51), raia wa Canada amekufa baada ya Parachuti alilokuwa akitumia kuruka angani kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kugoma kufunguka.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 28, 2019 kamishna msaidizi mwandamizi wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amethibitisha kifo cha mtalii huyo, kwamba kimetokea katika kituo cha Stella Point kilichopo katika mlima huo.
Amesema mtalii huyo alifika Septemba 20, 2019 kwa ajili ya kupanda mlima, leo asubuhi alitumia Parachuti kwa ajili ya kuruka angani ili kushuka chini ya mlima lakini iligoma kufunguka na kusababisha kifo chake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post