Rais
wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe atazikwa kwenye makaburi yaliyoko
kwenye kilele cha kilima, ambayo yamehifadhiwa makhsusi kwa watawala wa
Zimbabwe.
Bado
tarehe kamili ya maziko haijatangazwa na haijulikani ni lini mwili wa
Robert Mugabe utarejeshwa nchini kutoka Singapore alikofariki wakati
anapokea matibabu.
Mugabe
aliyefariki akiwa na miaka 95 atazikwa katika makaburi ya mashujaa wa
kitaifa kulikotengwa kwa raia wa zimbabwe waliyochangia pakubwa wakati
wa vita dhidi ya utawala wa wazungu .