Mwakyembe Afurahishwa Uanzishwaji Wa Shule Ya Michezo 'Kahama United Spots Academy'



Na Salvatory Ntandu
Waziri wa Habari Sanaa na Utamaduni, Dkt. Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa (Kahama United Sports Academy) kwa kuanzisha shule maalumu ya michezo yenye lengo la kuinua na kukuza vipaji vya mipira wa miguu hapa nchini.


Pongezi hizo amezitoa jana wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika hafla maalum ya uzinduzi wa shule hiyo na kusema kuwa endapo kila mkoa hapa nchini utaanzisha shule za michezo Tanzania itakuwa na hazina kubwa ya vijana wenye vipaji maalumu vya michezo tofauti tofauti ambayo iwasadia kupata ajira.


Amefafanua kuwa Michezo kwa sasa ni ajira hivyo kuwepo kwa shule hizo kutatoa fursa kwa wachezaji kuajiriwa na vilabu mbalimbali vinavyoshiriki mashindano ya ndani ya nchi na kimataifa kutokana na kupata maarifa sahihi katika shule hizo.


Waziri Mwakyembe amesema serikali itaendelea kuwaunga mkono wadau wote wa michezo watakaokuwa tayari kuanzisha shule za michezo ili kuhamasisha vijana kupenda kushiriki katika michezi mbalimbali na kuwawezesha kutojiunga na makundi hatarishi katika jamii.


Aidha Mwakyembe amekubali kuwachukua wachezaji wawili wa shule hiyo ambao ni pamoja na Delphinius Dikson,Raphael Kevin na Peter Nzogoya na kuwapeleka kufanyiwa majaribio katika timu ya taifa ya vijana ya Serengeti.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Usaji wa shule hiyo,Hamis Mgeja ameiomba serikali kuziwezesha shule hizo kwa kuzipa vifaa vya michezo vya kisasa ili kuendana na soka la ushindani hapa nchini.

Waziri wa Habari Sanaa na Utamaduni, Dkt. Harrison Mwakyembe akikata keki wakati wa uzinduzi wa shule ya Kahama United Sports Academy


Mwenyekiti wa bodi ya Usaji wa shule ya Kahama United Sports Academy, Hamis Mgeja akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule ya Kahama United Sports Academy

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post