Mwalimu
wa Shule ya Msingi Namagubu wilayani ukerewe Mkoani Mwanza, Joseph
Msafiri anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumjeruhi Mpenzi
wake Neema Kabulu kwa kitu chenye ncha kali (panga) kwa wivu wa mapenzi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea
septemba 6 majira ya saa mbili usiku katika nyumba ya kulala wageni
iliyopo eneo la Old Shinyanga, mjini shinyanga.
Amesema
Joseph akiwa katika maandalizi ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake
Neema nyumbani kwao walilala katika nyumba hiyo wakitokea ukerewe jijini
Mwanza lakini ilipofika usiku alimkata kwa na kitu chenye ncha kali
sehemu za usoni, tumboni na mkono wa kulia na Chanzo cha tukio hilo ni
wivu wa kimapenzi.
Kamanda
Abwao amesema Majeruhi anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa
Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya kutokana na kujeruhiwa katika
tukio hilo na wanaendelea kumshikilia Joseph kwaajili ya upelelezi.
Amefafanua
kuwa baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili ambapo eneo la tukio Jeshi la polisi wamepata panga
lililotumika kufanya tukio hilo, na Nguo zenye damu.