NBC YAJIKTA KUFANYA MABORESHO YA HUDUMA ZAO KWA DIGITALI





Watanzania wameaswa kuchangamkia fursa za huduma za kifedha zinazotolewa na Benki ya taifa ya biashara (NBC) zilizoongezwa thamani kwa njia ya mtandao ili kupata huduma hizo popote walipo na hivyo kuwarahisishia upatikanaji wa huduma ikiwemo nje ya nchi.

Akiongea kwenye halfa ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki ya Taifa ya biashara NBC Mkuu wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alisema kuwa kwa msingi huo usalama wenu tumeendelea kuulinda uliowasaidia kuongeza ufanisi kwa misingi ya utoaji wa huduma bora kwa jamii zitakazo saidia kutengeneza faida na myororo wa thamani kuongezeka.

Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikisaidia sana kwa kurudisha faida kwa jamii ili kukuza maendeleo ya nchi yetu jambo hilo limekuwa likisaidia sana ukuaji wa kiuchumi na kama mnao uwekezaji mpya karibuni sana Arusha kwa ni sehemu salama.

“Ni jambo jema sana kwa benki hii kuwakutanisha wateja na kuzungumza nao kuhusiana na maboresho ya benki yetu nasi serikali kama wadau wa benki hii tumeendelea kutoa huduma ya usalama kwa ajili ya maendeleo ya benki na taasisi zingine kuiga mfano huu”alisema Mkuu wa wilaya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa wateja wakubwa Nbc Linde Kapya kwenye hafla ya chakula cha jioni alisema kuwa kwa wateja wakubwa wa benki hiyo ni lengo lao kuwatambulisha wateja maboresho yanayofanywa na benki hiyo kurahisisha huduma kuwafikia wateja wao.

Alisema kuwa changamoto mbali mbali wameendelea kuziboresha ndio maana wanakutana na wateja wao kuona wamezipokeaje kwa lengo la kutoa huduma zinazokubalika kwa wateja wao na kuvutia wengine kutumia huduma za benki hiyo.

“Tumeendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwa muda wa miaka 50 sasa maoni yao tumekuwa tukiyafanyiakazi ili kuendelea kuboresha huduma zetu kwa lengo la kuongeza ufanisi na wigo mpana wa wateja wetu katika utoaji huduma zinazoendana na ulimwengu wa sasa”alisema Kapya.

Awali akiongea Meneja wa tawi la Benki hiyo mkoani hapa Miraji Msuya alisema kuwa siku hiyo ni muhimu sana kwa benki hiyo kukaa na wateja kwa kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma zao ikiwemo wateja wakubwa wakati na wadogo.

Alisema kuwa wao wapo kwa wateja zaidi kujua wao wanfikaje mbele ili kujua fursa zao kuweza kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma zetu zenye ubora uliosaidia kuendelea kukua siku hadi siku kwani taasisi zote ni watoto wetu.

Nae Christophe Msangule Meneja bidhaa na Teknolojia wa NBC alisema kuwa huduma zao zimejikita zaidi kidigitali na wamekuwa wakiziongezea thamani kwa kuwa wana mifumo mipya ambayo huduma za kibenki mteja wao ana uwezo wa kupeleka fedha nje akiwa ndani ya ofisi yake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post