Na Woinde Shizza,Arusha
Mkutano
wa 21 Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika unatarajia kuanza Septemba
15 mwaka huu Jijini Arusha na utajumuisha wakuuwa polisi kutoka katika
nchi 14.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi
(SACP)David Misime alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika ambapo
Rais John Magufuli atafungua mkutano huo Septemba 19 mwaka huu .
Alisema
kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo kutatanguliwa na vikao mbalimbali
vya wakuu wa vitengo vya Interpol na Septemba 16/17 kutakuwa na mkutano
wa wakurugenzi wa upelelezi (DCI)kutoka nchini 14 pia kutakuwa na kikao
cha kamati ndogo cha wataalam wa mafunzo , wataalamu wa sheria na kikao
cha wa kujadili unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha Kuzuia na
Kupambana na ugaidi
Alisema
kauli mbiu kuimarisha ushirikiano na ubunifu katika kupambana na
uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo makosa ya kimtandao,ugaidi"
Alisema
maandalizi ya mkutano huo yapo vizuri chini ya msimamizi wa Mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo na jana wamekaa na wataalamu wa Interpol kutoka
Kenya ambao wamefanya kikao
Pia
watawapeleka wageni wa mkutano huo chuo cha Polisi Moshi kwaajili ya
kuona madarasa mapya na majengo ya hosteli lengo ni kuongeza wanafunzi
wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali
Pia
watawapeleka Gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro
kwaajili ya kujionea utengenezaji wa viatu vinavyotumiwa na majeshi
mbalimbali huku wengine wakuu wa Majeshi ya Polisi wakienda kutembelewa
Hifadhi ya Ngorongoro kujionea Utalii uliopo Nchini
Alisema
Septemba 20 kutakuwa na kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani kutoka
nchi hizo na alitoa rai kwa watanzania kuimarisha amani na utulivu
Mada
zitakazojadiliwa ni kuongeza ushirikiano kwa uhalifu unaovuka mipaka
ikiwemo mikakati ya kutoa mafunzo kwa askari wao kwani hivi sasa Sayansi
na teknolojia imekuwa pamoja na kuangalia maazimio waliyoyatekeleza
katika kikao kilichofanyika mwaka jana nchini Sudani huku Mkuu wa Jeshi
la Polisi Nchini (IGP)Sirro akikabidhiwa rasmi uenuenyekiti mkutanor huo