Na Francis Godwin, Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Alli Hapi amewapongeza wakurugenzi wa halmashauri , wakuu wa wilaya zote na kukamilisha zoezi la kukimbiza mbio za mwenge wa Uhuru salama huku akiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuchunguza miradi iliyokataliwa na mwenge na kuchukua hatua za kisheria .
Hapi alitoa agizo hilo jana katika kijiji cha Idofi wakati akikabidhi mwenge kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole sendeka .
Alisema kuwa kazi kubwa imefanywa na viongozi hao hivyo wanastahili pongezi kwa kukamilisha zoezi hilo salama na kuwa mwenge umehitimisha mbio zake leo kwa kukimbizwa kwenye wilaya zote tatu na Halmashauri tano kwa miradi 26 ya kimaendeleo yenye thamani ya shilingi 7,650,102,463.20 kupitiwa na mbio za Mwenge .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi (kulia) akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka jana baada ya mwenge kumaliza mbio zake mkoani Iringa |
Kijana mkimbiza mwenge wa uhuru Kenani Kihongosi ambae ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa akizungumza na katibu tawala wa mkoa wa Iringa Hapines Seneda na mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi |
"Miradi 24 na shughul
Kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika miradi hiyo anaagiza TAKUKURU na vyombo vya dola vilivyopo mkoani Iringa kufuatilia na kufanya uchunguzi dhidi ya mapungufu hayo ili waliohusika wapelekwe kwenye vyombo vya sheria.
"Kati ya miradi iliyokataliwa na mwenge mwaka huu mradi miradi mitatu huu mradi mmoja ni mradi ambao ulizinduliwa na mwenge wa uhuru mwaka jana ila mwaka huu umekataliwa hivyo vyombo vya usalama fanyeni kazi ya kuchunguza na kuchukua hatua pale inapohitajika na kama wahusika wapo nao wachukuliwe hatua"
Hapi alisema kuwa mwenge wa uhuru katika mkoa wa Iringa ulitoa ujumbe maalumu wenye kuhamasisha wananchi kutunza vyanzo vya maji na kuwekeza katika sekta ya maji na kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa chini ya kauli mbiu isemayo Maji ni haki ya kila mtu tutunze vyavyo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa .
Aidha ujumbe wa kudumu ni kataa Rushwa jenga Tanzania ,tujenge maisha yetu ,jamii yetu na uhuru wetu bila dawa za kulevya ,pima jitambue Ishi na niko tayari kutokomeza malaria wewe Je?.
Hivyo alisema kupitia mwenge wa uhuru wananchi walipata elimu juu ya maambukizi ya UKIMWI ,kupambana na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya na elimu mbali mbali kulingana na kauli mbiu ya mwenge.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Alli alipongeza jitihada za wananchi na viongozi wa mkoa wa Iringa kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo na kujitokeza katika mbio za mwenge na kukesha na mwenge.
Hata hivyo alisema lengo la mwenge ni kuhakiki ubora wa miradi hiyo kabla ya kuzindua ili kuona ni miradi bora inayoendana na fedha zilizotolewa na serikali ya Rais Dkt John Magufuli .
Aidha aliwataka wananchi kuwapuuza wapinzani ambao wamekuwa wakiisema vibaya serikali kuwa haijafanya kitu wakati uhalisia wananchi wameuona kwa miradi mikubwa yanayoendelea kujengwa nchini .