Spika Pelosi aanzisha uchunguzi rasmi kuhusu madai ya Ukraine yanayomuhusisha Trump


Pelosi and Trump
Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi (kushoto)amesema kuwa rais Trump "lazima awajibike



Chama cha Marekani cha Democrats kimeanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusiana na madai kwamba alitaka usaidizi kutoka kwa taifa la kigeni ili kumuangamiza hasimu wake wa kisiasa.

Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrat Nancy Pelosi amesema kuwa rais "lazima awajibike ".

Bwana Trump anakanusha madai hayo na amezitaja juhudi za kumtuhumu kama " hila chafu'' dhidi yake .

Huku kukiwa na uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wafuasia wa Democrats juu ya uchunguzi huo unaoweza kumuondoa mamlakani, ikiwa utaendelea huenda usipitishwe na baraza la seneti - linalodhibitiwa na wabunge wa chama cha Trump cha Republican.

Mzozo huo ulichochewa na ripoti za jasusi aliyefichua malalamiko kuhusu simu ambazo rais Trump alimpigia mwenzake wa Ukrain rais Volodymyr Zelensky.
Kuhusu ni nini hasa alichosema limesalia kuwa lisilo wazi , lakini Democrats wanamshutumu Bwana Trump kutishia kusitisha msaada wa kijeshi kuishinikiza Ukraine kuchunguza madai ya rushwa dhidi ya makamu wa rais wa zamani Joe Biden na mtoto wake wa kiume Hunter.

Bwana Trump amekiri kuwa alimzungumzia Joe Biden na Bwana Zelensky lakini akasema alkuwa tu akijaribu kuitaka Ulaya iingilie kati kutoa msaada kwa kuitishia kusitisha msaada wa kijeshi.
Speaker of the House Nancy Pelosi
Awali Spika Nancy Pelosi alikataa kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya rais
Bi Pelosi amesema nini ?
Bi Pelosi alisema kwua Bwana Trump amefanya kosa la "ukiukaji wa sheria ", na kuyataja matendo yake kama "uvunjaji wa wajibu wake wa kikatiba''.

"Wiki hii rais Trump alikiri kumuomba rais wa Ukraine kuchukua hatua ambazo zitamnufaisha kisiasa ," alisema, na kuongeza kuwa : "Rais lazima awajibishwe."

Kama Spika wa bunge, Bi Pelosi ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Democrat. Bi Pelosi awali amekuwa akipinga miito ya kutaka amuondoe madarakani rais wa Republican akidai juhudi za aina hiyo zinaweza kuimarisha uungaji mkono kwa Trump.
Bwana Biden amekanusha kufanya kosa lolote na pia anaunga mkono juhudi za kumfanyia upelelezi rais iwapo hataonyesha ushirikiano katika sakata hiyo dhidi yake.

Uchunguzi dhidi ya Bwana Trump "unaweza kuwa janga ", alisema Bwana Biden . "Lakini janga alilojitengenezea mwenyewe ." Kwa sasa ndiye mtu aliyemstari wa mbele katika kukabiliana na Bwana Trump katika uchaguzi wa 2020.
Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia)
Trump anashutumiwa kuwashinikiza viongozi wa Ukraine kumchunguza hasimu wake kisiasa Joe Biden(kulia

Bwana Trump alijibu vipi ?
Katika msururu wa jumbe zake za Bwana Trump alisema Democrats wana lengo la "makusudi la kuharibu " ziara yake katika Umoja wa Mataifa " kwa taarifa zaidi za hivi punde za hila chafu za takataka ".

"Hata hawajaona ujumbe ulioandikwa wa simu wanazodai nilipiga . Hila tupu !" aliongeza
Aliahidi kutoa ujumbe wa mazungumzo baina yake na mwenzake wa Ukraine kwa maandisi siku ya Jumatano ili kuonyesha kuwa "ulikuwa unafaa kabisa".
Katika jibu lake , Kiongozi wa Republican bungeni Kevin McCarthy amesema : " ilitokea Pelosi akawa Spika wa bunge hili , lakini hazungumzi kwa niaba ya Wamarekani inapokuja katika suala hili ."
"Hawezi kuamua peke yake kuwa tutakuwa katika upelelezi ," alisema.

Wakati huo huo , kaimu mkurugenzi wa shirika la taifa la ujasusi nchini Marekani , Joseph Maguire, amekataa kushirikisha bunge la Congress ripoti ya mtu aliyefichua taarifa za shutuma dhidi ya Trump. Anatarajiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya umma ya ujasusi siku ya Alhamisi.

Ni nini kitakachofuata?

Tangazo la Bi Pelosi linatoa ruhusa rasmi kwa kamati kuchunguza mazungumzo ya simu za rais wa Marekani na kiongozi wa Ukraine l na kubaini ikiwa alifanya kosa linaloweza kusababisha afanyiwe uchunguzi wa kumondoa madarakani.

Katika tangazo lake Bi Pelosi alisema kuwa kamati nyingine sita zinazofanya uchunguziwa masuala mengine dhidi ya Trump nzitaendelea na uchunguzi wao chini ya uchunguzi wa sasa.

Ikiwa uchunguzi huu utaendelea, Bunge la wawakilishi litapigia kura mashtaka yoyote yatakayobainika na kwasababu Democrats ndio wengi katika bunge la congress wanaweza kupitisha umuzi wa kumshtaki.

Hata hivyo maamuzi hayo yanaweza kupelekwa katika bunge la Seneti ambako theluthi tatu ya wabunge inahitajika kupitisha maamuzi - na huko Republicans wataweza kuzuwia mashtaka.

Kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la A YouGov ilisema kuwa 55% ya Wamarekani wangeunga mkono kushtakiwa kwa Trump ika ingethibitishwa kwamba Trump alisitisha msaada wa kijeshi kwa ukraine ili kuwashinikiza maafisa wa nchi hiyo kumchunguza Joe Biden. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post