MAMENEJA WA TANESCO WAKUTANA ARUSHA KUJADILI TATIZO LA KUKATIKA UMEME MARA KWA MARA


Na Woinde Shizza, APC BLOG, ARUSHA

SHIRIKA la umeme Tanzania limesema kuwa  katizo la umeme la mara kwa mara linaloendelea hivi sasa kikomo chake kitakuwa mwaka 2025 na wananchi watakuwa wamesahau kabisa shida hiyo.


Hayo yamebainishwa na kaimu Naibu mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco )Mhandisi Raymond Seya wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo wahandisi wa matengenezo na  Mameneja wa shirika hilo wa Mikoa na kanda iliokuwa ikifanyika leo Jijini Arusha.

Mhandishi Seya kama shirika wako kwenye mikakati ya kuboresha zaidi utendaji wake kwa viwango vya kimataifa  vya  umeme ambapo umeme unatakiwa kutokatika kabisa na kama utakatika ukatike mara nne kwa mwaka na mkakati wa kutekeleza hayo umeanza leo katika kikao hicho.

Anasema wamekuwa wakiamini kuwa kikao hicho ni sehemu ya mwarobaini wa tatizo la umeme kukatikati mara kwa mara  na kwamba wahandisi hao  wameshakusanya matatizo yote na wapo hapo kuyapatia ufumbuzi.

"dhana kamili ya semina hii ni moja ya kazi ambayo wahandisi hawa watafanya ni kuhakikisha kwamba umeme haukatiki kabisa kwa sababu umeme unavyokatika hata kwa dakika moja ni hasara kubwa sana, kwanza kabisa umeme ukikatika unailetea serikali hasara kwani inakosa pesa, kwa upande wa viwanda vyetu navyo vinapata hasara kwa mfano kiwanda cha kutengeneza plastiki umeme ukikatika ghafla kama wanaendelea kuzalisha wanakuwa wameharibu  matirio yale waliokuwa wanatengenezea kwa hiyo hii itachangia kufukuza wawekezaji wa viwanda,”amesema.





Amesema kuwa wanataka kuhakikisha kila mwananchi anapokea na kunufaika na umeme wa uhakika lakini pia katika sera yetu ya Tanzania ya viwanda haiwezi kufanyakazi vizuri kama umeme utakuwa sio wa uhakika ,na pia kama umeme hautakatika mara kwa mara pia tutawavutia wenye viwanda kuja kuwekeza hapa nchini kwetu  na wakija kuwekeza serikali yetu itaongeza mapato , na pia ajira zitaungezeka kwa wananchi wetu.

Kwa upande wa muhandisi Mahende Mgaya meneja mwandamizi wa usambazaji  wa shirika la umeme Tanzania anasema kuwa wamechukua kumbukumbu za chanzo cha kukatika umeme za kuanzia mwaka 2015 iliopita wakazichakata na kujua tatizo ni nini na baada ya hapo wakatengeneza mkakati ambao wameugawa kwa awamu tatu ambapo  awamu ya kwanza wataangalia tatizo, watalifanyia kazi  na mwisho watahakikisha tatizo limeisha kabisa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post