TFS MUHEZA NA KILOSA YAKUSANYA BILIONI 1.9 YA MAUZO YA MITI


Mkurugenzi wa TFS Mohamed Kilongo akizungumza kuhusiana na mnada wa mazao ya misitu uliofanyika  Longuza wilaya ua Muheza mkoa wa Tanga

Na.Vero Ignatus,Muheza.

Serikali imekusanya zaidi ya sh 1.9 Billioni kupitia  mauzo ya mazao ya misitu yaliyouzwa kwa njia ya mnada katika Wilaya za Kilosa Mkoa wa Morogoro na Muheza mkoa wa Tanga.

Mohamed Kilongo ni Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi ya Misitu wa Wakala wa huduma za misitu (TFS),Akizungumza wakati wa mnada kwenye shamba la Longuza,  amesema kuwa   kisasi hicho cha fedha kimekusanywa kwenye misitu ya Mtibwa Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro na Longuza lililopo Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.

Amesema kuwa zaidi ya sh 453.milioni zilikusanywa katika mnada
wa shamba la Mtibwa na zaidi ya sh 1.5 Bilioni zilipatikana kwenye uuzwaji wa miti ya shamba la Longuza baada ya kuuzwa ujazo wa 2100 kati ya elfu 12 zilizopangwa kuuzwa.

Aidha  amesema Serikali imepanga kuuza miti ya eneo la ujazo wa Mill 1.62.8 katika misiti yake 13 iliyopo kote nchini na kwamba miti iliyouzwa Longuza ni ya aina ya Misaji yenye umri wa miaka 48.

Amesema  mwaka 2012 mpango wa uuzwaji wa mazao ya misitu ulianza  mara baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Misiti nchini (TFS)ambapo aina tatu za kuuzwa mazao hayo zinatumika ikiwemo utumaji maombi yaani mnunuzi,kutangazwa kwa mnada na mali zitakazo uuzwa na ule wa mazungumzo na mnunuzi husika.

Dkt. Cellina ni afisa misitu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Misitu na Nyuki, Mongo amesema minada hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya misitu sura 323, kanuni  za misitu za mwaka 2004 na tangazo la serikali namba 255/2017.

Dkt.Mongo ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mnada huo alisema sheria
hiyo inaelekeza namna ya uuzwaji wa miti hiyo aina ya misaji na kwamba
utazingatia  hali ya bei ya soko iliyopo.

Yusuff Ngage wa Kampuni ya Prime Timber iliyoshiriki mnada huo aliipongeza TFS kwa kuuza misitu kwa njia ya mnada kwa kuwa kila hatua inafanyika kwa uwazi na hivyo kuondoa malalamiko ambayo yalikuwa yakipokea awali

"Utaratibu huu utasaidia kuboresha viwanda vya ndani ambavyo vinahitaji bidhaa hizi kwa wingi ili kutekeleza kwa vitendo mpango wa Taifa wa uchumi wa viwanda".Alisema Yusuff.

Aidha Mnada huo uliendeshwa chini ya usimamizi wa viongozi waandamizi wa Idara ya Misitu ya Wiza.ra ya Maliasili na Utalii.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post