Joctan Agustino, Njombe
Wakala wa huduma za misitu
Tazanania TFS imekutanisha watu wenye ulemavu wa kusikia maarufu viziwi kutoka
mikoa mitano ya nyanda za juu kusini na kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo
katika utunzaji wa rasirimali za misiti na ufugaji nyuki ili kuwa na uwezo wa
kuhimarisha kipato cha familia zao.
Hatua hiyo imekuja baada ya kundi
hilo maalumu katika jamii za kitanzania kupaza sauti katika majukwaa ya umma
wakidai taasisi nyingi za umma na binafsi zimekuwa zikiwatenga katika masuala
mbalimbali ikiwemo kujumuishwa katika mafunzo yakuwaongezea ujuzi.
Akitoa ripoti ya utafiti ya 2015
iliyofanywa na TFS kaimu meneja wa nyanda za juu kusini Ebrantino Mgiye amesema
takribani hekta laki 275 za misitu zimeteketezwa nchini nyanda za juu kusini
pekee ikionekana kuchangia asilimia 16 kutokana na shughuli za kibinadamu
ikiwemo kuchoma mkaa, kilimo na uchomaji wa mioto na kwamba kuliemisha kundi
hilo muhimu kutasaidia kutunza mazingira yetu.
Mbali na kutoa elimu ya utunzaji wa
rasilimali za misitu TFS imeanza kutoka mafunzo ya ufugaji nyuki kwa kundi hilo
la walemavu ili waweze kuwa na uelewa kuhusu ufugaji huo ambapo utawapa fursa
ya kutengeneza kipato.
Awali akifungua mafunzo kwa niaba
ya mkuu wa mkoa wa Njombe , Dr George Katemba ambaye ni mkuu wa idara ya uchumi
na uzalishaji amesema wakala huo wa misitu umefanya jambo la maana kulitambua
kundi hilo maalumu na kulipa elimu ya utunzani wa rasirimali misitu na ufugaji
nyuki kwa kuwa limekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Kelvin Nyema ambaye ni katibu
mtendaji wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania TAMAVITA na Twasigwe
Mwalegwa mlemavu wanasema nyanda za juu kusini imekuwa na uharibifu mkubwa wa
mazingira na kwamba mafunzo hayo yatasaidia kutunza mazingira pamoja na
kujiajiri katika kilimo cha nyuki .
Katika hatua nyingine watu hao
wenye ulemavu wa kusikia wameziomba taasisi nyingine kulitambua kundo lao na
kulipa kipaumbele kama makundi mengine pindi wanapotoa fursa zikiwemo za
mafunzo na misaada mbalimbali. Washiriki 50 kutoka mikoa ya Rukwa, Songea ,
Mbeya,Njombe na Iringa