VYAMA VYA SIASA VYAONYWA KUPELEKA MAJINA YA WAGOMBEA WASIO NA SIFA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA



Na Ashura Jumapili, Bukoba
Serikali mkoani Kagera itakichukulia hatua kali  chama chochote cha siasa kitakachopeleka jina la mgombea asiyekuwa na sifa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 ,Novemba mwaka huu.


Onyo hilo limetolewa leo Septemba 12,2019 na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustine Kamuzora wakati wa kuapishwa kwa wateule wa usimamizi nane wa uchaguzi kutoka halmashauri zote za mkoa huo. 


Alisema mkoa umeshatoa maelekezo kuwa majina ya wagombea yatakayopelekwa kwa wasimamizi wa uchaguzi lazima awe raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.


Alisema wananchi wanayo haki ya kupinga mgombea ambaye uraia wake una mashaka .


"Chama kitakacholeta mgombea mwenye uraia unaotiliwa mashaka kitapoteza nafasi kwa sababu kanuni zinaonyesha sifa za mgombea ya kwanza no lazima awe raia wa Tanzania", alisema Prof.Kamuzora. 


Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika na hivyo kuwataka wananchi wawe walinzi dhidi ya watu wanaojipenyeza kugombea wasiokuwa na sifa hasa Wilaya za Ngara,Kyerwa na Missenyi.


Aliwaomba wateule hao wa usimamizi wa uchaguzi kusoma zaidi maandiko ili waweze kuelewa majukumu yao katika uchaguzi huo.


"Nimefarijika sana kuona nusu ya wateule ni wanafunzi wangu.Hakikisheni hamcheleweshi wala kuwa sehemu ya kusababisha matatizo",alisema Kamuzora.


Wateule hao wameapishwa na hakimu mkazi mahakama ya wilaya ya Bukoba Frola Kaijage.


Kaijage alisema wakienda kinyume sheria inachukua hatua ya kijinai na taratibu za kinidhamu.


Waliopishwa ni Costantino Msemwa kutoka Biharamulo mkuu wa idara ya Mipango takwimu na ufuataliaji,Babylus Mashauri kutoka halmashauri ya Bukoba mkuu wa idara ya Kilimo ,umwagiliaji na ushirika,Bukoba manispaa Richard Mihayo mkuu wa idara ya Mipango takwimu na ufuatiliaji.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post