Waziri Lugola Amtaka RPC Morogoro Arudi Kilimanjaro Haraka

WAZIRI  wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Hamis Issa kurudi Mkoani Kilimanjaro na kuhakikisha Mwananchi Hemed Mbaga anatolewa mahabusu kutokana na kubambikiziwa kesi.

Pia amemwagiza OCD wa Dodoma Mjini, Joas Steven kumpa orodha ya askari ambao wamekuwa wakiwabakizia kesi madereva  bodaboda na bajaji wa Dodoma ili aanze kushughuka nao.

Lugola ametoa agizo hilo jana Septemba 22,2019 katika bonanza lilofanyika uwanja wa shule ya msingi Chang'ombe jijini Dodoma baada ya  kukutana na waendesha bodaboda na bajaji ili kusikiliza kero zao.

Waziri Lugola amesema Julai  18,2019 Polisi mkoani Kilimanjaro walimkamata Mbaga wakati alipokwenda kuangalia mkusanyiko wa watu kufuatia bodaboda wawili kutelekeza fulushi la bangi.

"Maofisa wa halmashauri walikuwa wanapita hapo kuelekea kwenye makusanyo lakini walikuwa wa kwanza kufika na ndipo Mbaga akaja akitokea nyumbani lakini cha ajabu wakambambikiza kesi na kumweka mahabusu hadi leo," amesema Lugola.
 
Kwa mujibu wa Waziri, taarifa zilimfikia na akaagiza mtuhumiwa atolewe haraka mahabusu lakini cha ajabu hadi jana alikuwa hajatolewa huku RPC akihamishiwa Morogoro.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post