AGIZO LA RAISI LATEKELEZWA KAGERA, NI KUHUSU KUHAMA KWA HALMASHAURI.



Na Silvia A Mchuruza.
Kufuati agizo la Rais wa awamu ya tano  Dk.John Pombe Magufuri kuagiza halmashauri zote kuhama mjini na kwenda maeneo ya vijijini,  alipokuwa katika ziara ya kikazi  mkoani Rukwa katika wilaya ya sumbawanga mji mdogo wa Lahela ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa wananchi wanyonge.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya bukoba vijijini Mh. Murshid Ngeze kwa kushirikia na madiwa wa halmashauli hiyo wameafikiana kuhama haraka kutoka katika halmashauri ya manispaa ya bukoba na kwenda katika eneo lililopangwa kwa ajili ya halmashauli hiyo ikiwa ni kati ya halmashauri 31 ambazo azipo katika maeneo ya kiutawa.
Hata hivyo halmashauri hiyo iliweka watafiti hili kuhakikisha wanapata eneo linalofikikika kwa urahisi kutoka kata zote za halmashauri ambapo walipendekeza maeneo matatu ambayo ni eneo la kijiji Kanazi (BUJUNANGOMA),eneo la nyakatoke kata Rubale pamoja naeneo la Kyema ambapo ni msitu wa halmashauri hiyo.
Aidha nao watafiti hao waliweza kufanya kazi hiyo kwa kupima umbali wa kilimita na baadae kuwasilisha katika baraza la madiwani  ambapo madiwani hao waliweza kupiga kura na kulipendekeza eneo la kijiji Kanazi (BUJUNANGOMA) lililo na ukubwa wa ekali 60 na kusema kuwa eneo hilo linafikika kwa urahisi ambapo lipo karibu na mji wa Kemondo hivyo ni rahisi kwenye kufanya upangaji na upanuzi wa mji.
Vilivile nae mbunge wa jimbo hilo la Bukoba vijijini Jasson Rweikiza amepongeza juhudi za watafiti waliofanya kazi ya utafiti na kuweza kipata eneo husika na linalofikika kwa urahisi.
“Jambo hili la kuhama kwa halmashauri sio jipya tumepewa siku 30 hata hivyo nakumbuka kipindi cha nyuma aliwahi kuja Mh. waziri Mizengo Pinda aliwahi kusema ni kwanini tupo mjini ikiwa sisi ni watumishi tunaopaswa kufanyia kazi vijijini walipo wananchi tunaotakiwa kuwahudumia pia huko tunapo hamia kutakuwepo fursa za kwekeza kwa wafanya biasharanaamini tutalitekelea agizo la Rais wetu kwa sababu hata siku anatoa agizo hili nilikuepo pia”Alisema Rweikiza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post