LHRC YAKUTANISHA USTAWI WA JAMII, OFISI YA DPP, POLISI DAWATI LA JINSIA KUJADILI CHANGAMOTO WA UKATILI WA KIJINSIA KUONDOA VIKWAZO VINAVYOKATISHA TAMAA


Na Seif Mangwangi, Arusha 

KUTOKANA na mlolongo wa ngazi za maamuzi kwenye ufuatiliaji wa mashauri yanayotokana na ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake, watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kushindwa kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia na kujikuta wakiendelea kuumia pasipo kupata msaada.

Wakili Doto Joseph akiwasilisha mada kuhusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika mafunzo yanayotolewa chini ya kituo cha msaada wa kisheria na haki za binaadam LHRC yanayoendelea jijini Arusha


Hayo yameelezwa leo Oktoba 17, 2019 Jijini hapa na Afisa Programu anayeshughulikia ,masuala ya kijinsia, watoto na wanawake katika shirika la Msaada wa Kisheria na Haki za Binaadam (LHRC), Renatha Selemani.

Amesema kutokana na changamoto hiyo, kituo cha LHRC kimelazimika kutoa mafunzo kwa maafisa ustawi wa jamii, Maafisa polisi katika dawati la jinsia,  mawakili, Hakimu na waendesha mashtaka wa Serikali katika mafunzo yanayoendelea jijini Arusha kujadili namna ya kupunguza mlolongo huo na kesi hizo kuharakishwa.

Lilian amesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya matukio mengi ya ukatili wa kijinsia kutoripotiwa kwenye vyombo vya kimaamuzi kutokana na kuwepo kwa mlolongo mrefu wa ngazi za kimaamuzi na kuwafanya wanaotendewa vitendo hivyo kukata tamaa.

“Mfano dawati la jinsia polisi wamekuwa wakipokea matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hapa lazima wazichunguze kama zina tija au la, baada ya hapo wanapeleka kwa mwanasheria wa Serikali na yeye apitie awarudishie halafu ziandaliwe kupelekwa mahakamani,”anasema.

Anasema baada ya kupelekwa mahakamani na kesi kusomwa, mahakimu na wanasheria wanaanza kusikiliza kesi ambazo pia hutegemea ushahidi na hivyo kufanya kesi kuchukua muda mrefu jambo ambalo limekuwa likikatisha tamaa.

Kwa upande wake Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu, Dotto Joseph amesema suala la ukatili wa kijinsia ni suala pana ambapo wakati mwingine masuala hayo yamekuwa yakifanyika katika ngazi ya familia kwa mume kumpiga mkewe na hivyo kumalizana nyumbani bila kuripoti mashauri hayo kwenye ngazi za kimaamuzi.

Amezitaja changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa ili kurahisisha uendeshaji wa mashauri hayo kuwa ni pamoja na kutolewa elimu ya mambo yanayopelekea ukatili wa kijinsia, kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sheria pamoja na kukomeshwa kwa mila potofu.

Kwa upande wake Afisa wa Polisi kutoka kanda maalum ya Tarime, Claud Mtweve pamona na Lilian Mugwe Afisa Ustawi wa jamii Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wamesema ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ikiwemo wajane kulazimishwa kuolewa baada ya kufiwa na waume zao umekuwa ukichangiwa na mila na desturi ambazo jamii imekuwa ikizirithi kutoka kwa wazazi wao.


Afisa Program masuala ya jinsia, wanawake na watoto wa LHRC Renatha Seleman  akimsikiliza mtoa mada katika mafunzo hayo kuhusu ukatili wa kijinsia
  
Washiriki wa mafunzo ya ukatili wa kijinsia wakimsikiliza mwezeshaji Doto James (hayuko pichani), akieleza mazingira yanayosababisha watu wengi kutofikisha mashtaka yao 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post