MAKONDA AKABIDHI MILIONI 40/- KWA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA...


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah. Wakicheza na watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40 Walipotembelea  

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akicheza na mmoja wa watoto kati ya 20 leo wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na baadhi ya wazazi wa watoto 20 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40.
Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bi. Loveness Hoyange  akizungumza na mmoja wa wazazi wenye watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete(JKCI)kwa ufadhili wa kampuni ya Puma Energy wenye thamani ya shilingi milioni 40.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akicheza na mmoja wa watoto kati ya 20 leo wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40. Kushoto ni Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah. Walipotembelea  taasisi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na wazazi wa baadhi ya watoto kati ya 20 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40. Kushoto ni Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah. Walipotembelea  taasisi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Profesa Mohamed Janabi na wazazi wa watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wakiwa katika picha ya pamoja.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru Kampuni ya PUMA Energy kwa kutimiza ahadi ya kuchangia Sh. Milioni 40, kwa ajili ya kuchangia matibabu ya moyo kwa watoto 20 wanaotibiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya makabidhiano ya fedha hizo leo Oktoba 3,2019 akiwa katika taasisi hiyo Makonda amesema kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo kurudisha tabasamu kwa watoto wanaosumbuliwa na moyo haina budi kuungwa mkono na kila mwenye uwezo.

“Wenzetu PUMA Energy wameamua kutuunga mkono, tutambue matibabu ya moyo ni mzigo mzito kama ukisimama nao peke yako, lakini ukipata wa kukushika mkono utauona mwepesi,” alisema.

Amesema anamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kusimamia vema sekta ya afya na hasa matibabu ya watoto na wagonjwa wengine wanaosumbuliwa na moyo.

“Serikali inatoa mchango mkubwa katika kurahisisha matibabu ya moyo ambayo ni ghali sana, awali ilikuwa lazima mgonjwa apelekwe India, lakini sasa serikali inaokoa fedha nyingi kwa kuwafanyia upasuaji na kuwawekea vifaa wagonjwa hapa hapa nchini,” amesema Makonda.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah amesema wamejionea kazi kubwa inayofanywa na JKCI katika kuokoa maisha ya Watanzania na hasa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo ambao tayari walishapoteza matumaini lakini kupitia taasisi hiyo wamerudisha matumaini ya watoto hao kuishi.

Dhanah amesema anatambua fedha ambazo wamechangia kwa ajili ya matibabu yasaidia kutibu watoto 20 na kuongeza wataendelea kushiriki hatua kwa hatua kusaidia watoto wenye mahitaji na hasa ya kufanyiwa matibabu ya moyo.

“Mnafanya kazi kubwa ya kurudisha maisha yaliyokuwa hatarini kupotea, vilevile ninampongeza Mkuu wa Mkoa Makonda kwa kusimamia hili kwa umakini.Tunafahamu wazazi wa watoto hawa hakuwa na fedha za kugharamia matibabu haya lakini PUMA Energy tutaendelea kuunga mkono hatua kwa hatua,”amesema Dhanah.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed Janabi amesema kuwepo kwa taasisi hiyo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa fedha za Serikali kwa kuwa awali gharama za mtu mmoja kufanyiwa upasuaji wa moyo nchini India ilikuwa dola za Marekani 15,000 ambazo ni zaidi Sh.milioni 30.

“Kwa wagonjwa 200 tuowafanyia upasuaji ingetugharimu zaidi ya sh.bilioni 9.4, hawa watoto mnaowaona hapa wamechangamka baada ya kufanyiwa upasuaji, walipokuja walikuwa wanyonge kwa sababu ya maumivu waliyokuwa nayo,” amesema Profesa Janabi na kuongeza:

“Vilevile itambulike kuwa hapa hatutibu wagonjwa wa Tanzania tu bali wapo wengine kutoka Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Malawi.”

Mmoja wa wazazi waliopeleka wagonjwa katika taasisi hiyo ambao wamepata msaada wa Mkuu wa Mkoa Makonda, ni Joyce Cosmas kutoka mkoani Kigoma ambaye amempeleka mtoto wake Aida Mfumya ambaye aliugua kwa muda mrefu bila kujua kitu gani kinamsumbua.

“Nimetoka Kigoma karibu na mpaka wa Burundi, wengi wanapopimwa na kubainika watoto wao wanasumbuliwa na moyo wanashindwa kuja Dar es Salaamkwa sababu ya gharama kubwa, lakini kupitia Mkuu wa Mkoa Makonda nimefanikiwa kupata matibabu,” amesema Cosmas.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post