MKURABITA YATAKIWA KUHAKIKISHA HATIMILIKI ZA KIMILA ZINATUMIKA KUWAPATIAMIKOPO WANUFAIKA WA MPANGO HUO ILI WAJIENDELEZE KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika mkoa wake jana kabla ya Naibu Waziri huyo kuanza ziara ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Tunduma mkoani Songwe jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)na kuzungumza na watumishi
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi, Bw. Kelvin Joseph alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuwaunganisha wanufaika wa MKURABITA na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na kujiinua kiuchumi wakati Naibu Waziri huyo aliposimama kukagua utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango huo.

Aaron Mrikaria, Songwe, 

Watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wametakiwa kuratibu taasisi za fedha zenye  utayari wa  kuwapatia mikopo wanufaika wa Mpango huo wenye hatimiliki za kimila ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowawezesha kuinua kipato na kuboresha maisha yao.
Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Mhe. Dkt. Mwanjelwa alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanufaika wa Mpango huo katika Kijiji cha Naming’ongo ambao wamesema wanashindwa kutumia hatimiliki za kimila kupata mikopo kutokana na kukosa mwongozo na utaratibu wa upatikanaji wa mikopo kwenye taasisi za fedha, licha ya hatimiliki hizo kupunguza migogoro ya ardhi.
“Nawapa wiki mbili mnipe majibu ya taasisi za fedha zitakazokubaliana na Serikali kutoa mikopo kwa kutumia hatimiliki za kimila, na kuongeza kuwa elimu kwa umma itolewe ili wananchi waliorasimishiwa mashamba na maeneo ya biashara wajue taratibu za kupata mikopo kwenye taasisi za fedha zilizo tayari kutoa mikopo hiyo,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Watendaji wa MKURABITA kuharakisha zoezi la kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi waliorasimishiwa ardhi, ikizingatiwa kuwa mchakato wa zoezi hilo huishia wilayani hivyo hakuna sababu ya ucheleweshaji.
“Kama mwananchi ameshatekeleza taratibu zote za urasimishaji, kuna haja gani ya kusumbuliwa wakati upatikanaji wa hatimiliki za kimila ni makubaliano ambayo yanakamilika katika ngazi ya kijiji na si wizarani,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kuona mashamba ya mpunga ya wanufaika wa MKURABITA wa Kijiji cha Naming’ongo na kuwapongeza kwa kilimo cha kisasa.
Jumla ya mashamba 776 yamerasimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe ambapo kati ya hayo, hatimiliki za kimila 527 zimeshatolewa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post