RUZUKU YA TASAF YABORESHA MAISHA YA WANAKIJIJI WA MKWANDA

1.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.   Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bw. Adam S. Mboka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.   Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bi. Aisha Jongo akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.   Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bw. Issa Shaban Mfaume akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisoma bango linaloutambulisha Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na wanufaika 82 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru alipoutembelea mradi huo kwa lengo la kujionea shughuli zinatofanywa na wanufaika hao.
1.   Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na wanufaika 82 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametembelea mradi huo.



Na James K. Mwanamyoto, Tunduru

Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru wamekiri kuboresha maisha yao baada ya kupokea ruzuku kupitia Mpango huo unaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuzinusuru kaya maskini ambazo zinahitaji msaada wa kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya wanufaika wa Mpango huo wameeleza hayo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) na wanufaika hao, uliofanyika katika kijiji hicho wenye lengo la kubaini mafanikio na changamoto za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Akitoa shuhuda wakati wa mkutano, mmoja wa wanufaika Bi. Aisha Jongo amesema TASAF imemuwezesha kuboresha makazi yake kwa kuezeka bati kwenye nyumba yake na kujenga nyumba nyingine ya bati.

“Awali nilikuwa nikiishi kwenye nyumba ya nyasi, nilipoanza kupokea ruzuku nilianza kununua bati moja moja mpaka zikatimia ishirini na kupaua nyumba yangu na kafanikiwa kujenga nyumba nyingine ya bati”, Bi. Jongo amefafanua.

Bi. Jongo ameongeza kuwa, kupitia TASAF ameweza kununua sola inayomuwezesha kupata umeme wa uhakika, hivyo ameachana rasmi na matumizi ya kibatari.

Naye, Bw. Issa Shaban Mfaume amesema yeye na wazazi wake wamenufaika na Mpango kiasi cha kuweza kujenga nyumba wanayoishi sasa, hivyo TASAF imekuwa na manufaa kwani wanaishi kwenye nyumba iliyoezekwa kwa bati.

Bw. Mfaume amemthibitishia Mhe. Mkuchika kuwa, awamu ya pili ya Mpango imemuwezesha kuwa na bwawa la kufugia samaki linalomuingizia kipato na hatimaye kuendesha maisha yake na ya familia yake vizuri.

“Hamasa na elimu ya kuanzisha bwawa langu la samaki nimeipata kupitia Mradi wa Bwawa la Samaki la kijiji cha Mkwanda ambalo ni la walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini”, amesisitiza Bw. Mfaume.

Akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuzungumza na wanufaika hao, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius Mtatiro amewaasa wanufaika hao kubuni miradi mbalimbali itakayowawezesha kutumia vema ruzuku wanayoipata kuondokana na umaskini.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amewapongeza wanufaika hao kwa kutumia vizuri ruzuku kuboresha maisha yao, na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ruzuku kupitia Mpango huo ili kutekeleza azma ya kuzinusuru kaya maskini.

Mhe. Mkuchika amewatembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post