Ahmed Mahmoud/Arusha
Naibu Katibu Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Thembinkosi Mhilongo amesema umoja huo umedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya hiyo
Hayo yameelezwa leo na Naibu Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana na Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii katika nchi hizo za Ukanda wa Kusini mwa bara la Afrika (SADC).
Dkt Mhilongo pia amesema nchi za SADC zimejipanga kuangalia kwa kina suala la Viumbe na Mimea vamizi katika nchi hizi wanachama pamoja na Wanyama ambao wako katika hatari ya kutoweka katika nchi hizo.
Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao wenye dhamana ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha wanaangalia kwa kina Itifaki na Mikataba inayohusu Sekta hizo tatu katika nchi Wanachama za SADC
Amesema Mkutano wa Mawaziri hao ni muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mataifa ya SADC hivyo amewataka wakati wa Mkutano huo kupima na kuangalia kwa kina Sera na Itifaki zinazosimamia Sekta hizo tatu ambazo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa mataifa hayo.
Mbali na kuangalia masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao kuhakikisha wanaangalia kwa Kina Sheria zote zinazosimamia na kuongoza Sekta hizo katika Jumuiya.
Amesisitiza kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama za SADC na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yanalenga katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika nchi za SADC
Nchi za SADC imebahatika kuwa na raslimali lukuki zikiwemo za Wanyamapori, misitu, Uvuvi rasilimali ambazo ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya nchi wanachama za SADC.
Amewataka Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki ya SADC inayohusu umuhimu wa kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori
Pia amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika
Naibu Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba historia kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita
Amesema SADC iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Keneth Kaunda wa Zambia, Rais Somora Machel wa Msumbiji, Rais Agustino Neto wa Angola na Rais Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyo iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC
Aidha Mkataba wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia kwa ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gaboro Nchini Botswana
Kukosekana kwa Visa moja kwa Watalii ulaya wanapokuja katika ukanda huu wa kusini mwa nchi za kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa