SAMIA ataka SADC kutenga fedha zaidi,wataalam kukabiliana na uharibifu wa mazingira

Na Claud Gwandu,Arusha

MAKAMU wa Rais,Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi wanachama wa Jumiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutenga fedha zaidi na wataalam wa masuala ya mazingira ili kuhifadhi mazingira na kuokoa rasilimali ilizobarikiwa nchi hizo.
Mawaziri pamoja na Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. wakimsikilioza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akifungua Mkutano huo leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo umefunguliwa leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa SADC  unaojadili kuhusu Mkakati  wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori  pamoja na hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Baada ya kufungua Mkutano huo  leo Octoba 25,2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa AICC Jijini Arusha.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Akifungua mkutano wa mawaziri wanaosimamia sekta za mazingira,maliasili na utalii wa  jijini hapa leo,Makamu wa Rais alisema kasi ya uharibifu wa mazingira ni kubwa kuliko  jitihada zinazofanyika katika kuhifadhi na kuokoa.

‘’ingawa nchi za SADC zimebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi,bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo uchafuzi wa mazingira,uharibifu wa mifumo ya maisha ya viumbe wa majini,unaribifu wa misitu,upotevu wa makazi ya wanyamapori na bioanuai hivyo jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kuokoa na kuhifadhi mazingira,”alisisitiza na kuongeza:

“Ni jambo la kusikitisha kuona kasi yetu ya uharibifu wa mazingira ni kubwa kuliko jitihada tunazofanya katika kuhifadhi na kuokoa rasilimali  tulizobarikiwa.Ili tuweze kukabiliana na changamoto hizi,sote tuna wajibu wa kulinda na kuokoa rasilimali tunaandaa mikakati inayoendana na protocals (itifaki) na Mipangombinu  ya SADC’’

‘’Lazima tuhakikishe tunatekeleza Mipangombinu hiyo kulingana na hali halisi za mazingira ya nchi zetu ikiwa ni pamoja na kutenga fedha zaidi na kuwa na wataalam wa masuala ya mazingira na pia kuzingatia kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kulinda na kuhifadhi rasilimali za mataifa yetu.”

Alisema kuwa nchi nyingi za SADC zina mipango mizuri ya kukabiliana na changamoto mbalimbali  za uharibifu na uchafuzi wa mazingira lakini  mipango hiyo hubaki kwenye mafaili na kuwa ni ya kinadharia zaidi kuliko kuzingatia uwezo wan chi kifedha na kitaalam.

Alitaka nchi wanachama wa SADC kutumia na kuzingatia mbinu na taaluma za kienyeji  zinazoweza kutumika kurekebisha uharibifu wa mazingira na pia kuwa na mfumo imara ya kusimamia utekelezaji wake

Alitaja athari zilizosababishwa na mabadiliko ya tabianchi kuwa ni pamoja na   mabadiliko ya hali ya hewa, bahari kumeza ardhi, mabadiliko ya misimu na viwango vya mvua  na kusababisha kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na mafuriko ya mara kwa mara na kuzuka kwa magonjwa ya milipuko.

Awali Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangwalla ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo wa mawaziri mkutano huo utaridhia mapendekezo yaliyowasilishwa na wataalam ambayo yanalinda maslahi ya Jumuiya.

Dk Kigwangalla alisema kuwa mkutano huo utajikita katika kupima utekelezaji wa Sera na Mikakati mbalimbali kuhusu mazingira,maliasili na utalii ikiwamo Itifaki ya SADC ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na utekelezaji wa Sheria na Mipango ya Kupambana na Ujangili na programu ya SADC ya maeneo ya uhifadhi yanayovuka mipaka.

Mikakati mingine itakayojadiliwa katika mkutano huo,ni itifaki ya SADC kuhusu usimamizi wa Misitu na Mkakati wa miisitu,itifaki ya SADC kuhusu Maendeleo ya Utalii na itifaki ya Jumuiya hiyo ya usimamizi  wa Mazingira endelevu,mkakati wa mabadiliko ya tabianchi na program ya kupambana na ueneaji wa jangwa.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post