SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO NA KERO ZINAZOKABILI VIWANDA VYA MAZIWA NCHINI

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeahidi kutatua changamoto kubwa inayokikabili kiwanda cha usindikaji wa maziwa cha Kilimanjaro fresh cha jijini Arusha kinachokabiliwa na changamoto ya ukubwa wa kodi ya ongezeko la thamani ambalo inabidi kushindwa kufikia uzalishaji mkubwa wa maziwa kama uhitaji wake ulivyo mkubwa kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh jijini Arusha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ullega amesema kwamba serikali kupitia wizara yake itahakikisha inaondoa changamoto hiyo ya tozo kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa usindikaji wa maziwa katika kiwanda hicho cha Kilimanjaro fresh Milk

Ullega amesema kwamba kiwanda hicho toka kuanzishwa kwake miezi 6 kimekua na mafanikio makubwa   "ili kupata mafanikio zaidi lazima mnunue kwa bei kubwa zaidi kutoka kwa wafugaji ambao watapata nguvu ya kuweza kuzalisha zaidi na kuongeza thamani ya uzalishaji wenye ubora unaohitajika,"amesema.

"Mmesema kuwa mtatoa motisha ya mitanda endeleeni na zoezi hilo kwa kuwa ni sehemu ya kuongeza motisha kwa wafugaji kuongeza uzalishaji kwenye bidhaa za maziwa hapa nchi nanyi kuweza kuongeza uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho na muendelee kufuata maagizo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja maziwawyanatengenezwa na kamanda cha KILIMANJARO Fresh  wakati alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na Ahmed Mahmoud,Arusha). 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda  cha  KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea  kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la  Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Ahmed Mahmoud, Arusha)
Naibu Waziri akipata maelezo
ya serikali kwa ajili ya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo,".

Alisema kuwa kiujumla wameeza vizuri katika uzalishaji wenye tija na kudai kuwa alipenda utoaji wao wa elimu kwa wafugaji katika  kuwapa elimu ya ulishaji wa chakula vizuri na kuwataka kurudia agizo la waziri mkuu kwa kiwanda cha maziwa Asas kwenye wiki ya maziwa Kilimanjaro kuandika barua wizarani  kuhusu malalamiko yao na wao watafanyia kazi kwa faida ya ukuaji wa tasnia

Awali akitoa maelezo ya Kiwanda hicho  mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Kilimanjaro Fresh  Irfhan Virjee alimweleza Naibu waziri changamoto zinazo mkabili katika uzalishaji wa maziwa kua ni pamoja na tozo ya kodi ya VAT.

Alisema kuwa mwezi wa kwanza mwaka 2020 wanatarajia kuzalisha lita zipatazo elfu 20 ambapo pia wanatarajia kuanza kuuza maziwa nje ya nchi ambapo walianza kuzalisha kuzalisha  lita elfu 3000 hadi sasa wanazalisha lita 800kwa siku.

Alisema kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa wafugaji  kutoka vyama vya ushirika ambapo huwauzia maziwa kwa kiasi cha shilingi 800 hadi kufikia shilingi 850 ambapo pia wakulima hupatiwa motisha kwa lengo la kuendelea kutunza mifugo kwa lengo la kuboresha mifugo kupata maziwa yalio na ubora wa hali ya juu .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post