UMEME WAWASHWA MPIMBWE

Meneja wa TANESCO mkoa wa katavi Felix Olang’ akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Katavi; kulia ni Meneja Mradi kutoka CRCEBG Arnold Nzali



Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akikata utepe kuashiria uzinduzi wa uwashaji umeme katika kata ya Maji Moto
…………………..
Na Mwandishi wetu,KATAVI
 
Zaidi ya wakazi 10,000 kati ya wakazi 54,000 wa kata za Maji Moto na Mamba katika halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi wanatarajia kunufaika na huduma ya nishati ya umeme baada ya kuwashwa kwa umeme katika kata hizo hii ikiwa ni mara ya kwanza kuwashwa umeme katika maeneo hayo tangu kupatikana kwa uhuru

Wakizungumza na waandhishi wa habari katika kampeni ya zima kibatari, zima jenereta, weka sola pembeni, wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuwapelekea huduma hiyo

Bwana Lameck Buzazi ni mmoja wa wakazi wa kata ya Mamba amesema atatumia huduma hiyo katika mambo mbalimbali ya kujiletea maendeleo
Baadhi ya vitu alivyotaja anaweza kufanya kufuatia uwepo wa umeme ni pamoja na kufungua saluni ya kiume, kununua jokofu kwa ajili ya biashara ya barafu kwa mkewe na kuongeza kuwa kwa sasa hata uangaliaji wa runinga utakuwa wa uhakika na hatasumbuka kufuata mpira katika runinga za maeneo ya baa

Mhandisi Felix Olang’ ni Meneja wa TANESCO mkoa wa katavi, amesema wanaendelea kuwaunganisha wateja kwa kushirikiana na mkandarasi wa kazi hiyo kutoka kampuni ya kichina ya CRCEBG
 amesema katika tarafa ya maji moto wana transifoma 13 na mpaka sasa ni tatu ndio zimekwishaunganishwa na wateja.
 
kwa upande wake meneja wa mradi kutoka kampuni ya kichina ya CRCEBG mhandisi Arnold Nzali amesema ndani ya siku thelathini watakuwa wamekamilisha kuunga transifoma zote 13 mara baada ya kufanya zoezi la uwashaji umeme katika baadhi ya makazi ya watu na kituo cha polisi maji moto mkuu wa mkoa wa katavi bwana Juma Homera amezitaka taasisi za serikali kuhakikisha zinajiunga na huduma hiyo.

Ametoa wito huo kufuatia kupokea taarifa ya kusuasua kwa taasisi kujiunga na huduma ya nishati ya umeme wa REA awamu ya tatu ambapo shule, zahanati, ofisi za serikali na taasisi za dini kutochukua fomu za kuwekewa umeme

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post