WANAFUNZI WAJERUHIWA BAADA YA KUPIGWA NA RADI WAKIWA DARASANI

Wanafunzi 39 wa darasa la nne shule ya Msingi Ihumilo wilayani Geita wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani.
 Radi

Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya Kaitila Murusuri ,amesema walipowakea wanafunzi 24 saa mbili asubuhi na kuwapatia huduma ya kwanza. 

''Tumepokea gari ya dharura kutoka zahanati ya karibu ya mkoma ikiwa imebeba wanafunzi wa shule ya msingi wapatao 24 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali ya kupigwa na radi , tulipowafanyia uchunguzi wengi wao walikuwa katika hali ya kawaida, tuliporidhika tuliwaruhusu lakini tulibaki na wengine watano, kikubwa ni kwamba walipata mshtuko''. Alieleza daktari Murusuri.


Taarifa zimesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza kwa sasa wanaendelea vizuri na tayari wengi wao wameruhusiwa kutoka hospitali.

Taarifa zinasema kuwa majira ya saa moja asubuhi ilipiga radi kali katika shule iliyopo maeneo ya Nzera katika halmashauri ya wilaya ya Geita. Watumishi wa afya waliwahi kuwasaidia kupata huduma ya kwanza.
 Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel
Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel amesema amezungumza na watoto hao wa darasa la nne.

''Ni majira ya mvua kipindi hiki radi hupiga wakati wote ukiwa barabarani radi inakufuata, ukiwa kwenye jengo lenye umeme radi inapiga, ukiwa kwenye jengo la umeme, kukiwa hakuna umeme radi inapiga kuna teknolojia inapaswa kutazamwa kuona ni namna gani tunaweza kujikinga na radi katika majengo yetu''. Amesema mkuu huyo wa mkoa.
 BBC

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post