Wanariadha waliokwenda Doha warejea, waponda uongozi RT



Na Lucas Myovela_Arusha.

Timu ya Taifa ya riadha hapa nchi imerejea usiku wa Oktoba 7,ikiwa imetokea Doha huko nchini Qatar baada ya kushiriki katika michuano ya riadha ya dunia iliyokuwaikifanyika katika mji wa  Doha.

Timu hiyo iliondoka nchini Oktaba 2 ,2019 ikiwa na jopo la watu wanne wanariadha watatu pamoja na kocha wa timu ndiyo waliweza kwenda kushiriki michuano ya dunia ya riadha ambapo michuano hiyo ilishirikisha wanariadha wa timu za mataifa mbali mbali.

Akiongeana na wanaandishi wa habari wakati wa kuwapokea wanariadha hao walipowasili katika ardhi ya Jiji la Arusha kutokea Doha wakipitia, Nairobi Nchini kenya Afisa utamaduni wa jiji la Arusha Benson Maneno ameeleza kuwa mpaka sasa timu hiyo inakila sababu ya kupongezwa kwa kila hali na mali kwa hatua waliyofikia.

Pia Benson Maneno ameleza kwamba licha ya changamoto mbali mbali walizokutana nazo wanariadha hao bado waliweza kuhimili hali ya hewa kutokana na joto kali walilo kutana nalo lakini bado wameiwakilisha nchi katika michuano ya dunia  na kuleta heshima kubwa baada ya nahodha wa timu hiyo kumaliza mzunguko wote.
Kwa upande wake kocha wa timu hiyo ya riadha hapa nchini Andrew Samson Panga,ameeleza kwamba licha ya joto kuwa kali hadi kufikia hatua ya wanariadha wengine kufunga barafu katika miili yao ili kupunguza joto pia walipata changamoto ya wanariadha wawili wa timu ya Taifa waliweza kuumia katika michuano hiyo na kupelekea kubakiza mkimbiaji mmoja kati ya watatu waliyo kwenda Doha.

"Vijana wetu wamepambana vya kutosha lakini changamoto tuliyopana ni vijana wetu kuumia ambapo Stephano Uche aliumia goti na badae mwariadha wetu Agostino Sulle alipata shida ya nyonga kwahiyo hawakuweza kufika mwisho au kumaliza mashindano na Alphonce Simbu aliweza kupambana hadi mwisho kama mlivyo weza kuona katika vyomba vya habari vya kimataifa kiukweli haikuwa kazi ndogo wala kazi rahisi". alisema kocha Samson.
"Kiukweli tuliyo fika pale tumejionea hali halisi ya pale Doha na kipindi tunakuja tulikuwa tunajiuliza tunarudi ingawa hatuna midani na niwashukuru sana kwa mapokezi haya mliyotupatia maana mmekuja kutupokea mbali na mmetukalibisha vizuri mapokezi haya yanatia moyo sana maana tumeshindwa lakini bado watanzania wapo na sisi ni jambo jema sana kushikamana". aliendelea kusema kocha Samson.

Pia nahodha wa timu hiyo ya taifa ya riadha Alphonce Simbu, ameeleza kuwa mbali ya wao kushindwa lakini ameweza kushika nafasi ya kumi na sita na kuweza kushiriki mashindano ya Olimpiki huko Tokyo 2020 na kuwataka viongozi wa riadha taifa kuwa wamoja na kuacha majungu na mapishano katika kuendeleza michezo ya riadha hapa nchi maana kwasasa kumekuwa na sito fahamu kubwa kwa viongozi hao tofauti na mwanzo.

"Kwa upande wangu nimshukuru kocha wetu kwa kuto kukata tamaa na kuwa nasisi bado hata tulivyo shindwa bado hajavunjika moyo ametupa moyo sana na kutusaidia kimawazo lakini kwasasa kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana kwa viongozi wetu wa riadha taifa ninaomba warudishe umoja wao maana hili jambo linatuvunja moyo wanariadha".alisema nahodha wa timu  Alphonce.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post