WAZIRI JAFO AWATAKA WAKURUGENZI WASIOTIMIZA UKUSANYAJI MAPATO KUJITATHIMINI.

Na.Faustine Galafoni.Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ma Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Selemani Jafo amewataka wakurugenzi wasiotimiza lengo la ukusanyaji mapato katika Halmashauri zao kujitathimini.

Waziri Jafo ameyasema hayo    Oktoba 21,2019 Jijini Dodoma  wakati akitoa taarifa ya mapato ya vyanzo vya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2019. .

Waziri Jafo amesema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja katika kipindi hiki imeonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeongoza kwa ukusanyaji mapato kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Bilioni 13.10,huku Mapato ya ndani kimkoa kwa kuzingatia wingi wa mapato Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 39.53

Pia Waziri Jafo amesema licha ya Serikali kuagiza ukusanyaji wa mapato kufanyika kwa njia ya kielektroniki lakini bado kuna Changamoto kwani kuna baadhi ya maeneo wanakusanya fedha na hawazipeleki benki hivyo kuwaagiza wakuu wa mikoa kusimamia suala hilo.


Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imekuwa ya mwisho katika pato ghafi kwa kukusanya Milion 35 kwa kipindi cha miezi mitatu na hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja wengine ambao hawajafanya vizuri kujitathimini huku uchambuzi ukionesha kuwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20,Jumla ya Halmashauri 54 kati ya Halmashauri 185 zimefanya vizuri kwa kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 25 ya makisio ya mwaka wa Fedha 2019/20.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post