MIPANGO MKAKATI DHIDI YA WAFUGAJI WAZINDULIWA ARUSHA


Na Mwandishi wetu APC BLOG, ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho  amezindua mpango mkakati wa  kibiashara wa wilaya mbili za simanjiro  na longido ambao unalenga  kuweka mipango ya namna  gani  wafugaji watajikwamua kiuchumi.

Akizungunza katika warsha ya uzinduzi wa mpango huo uliofadhiliwa na  mradi wa Maisha bora  kwa ushirikiano wa shirika la Trias Gambo amesema kuwa mpango huo utawezesha wafugaji wa wilaya hizo kuwa na thamani  hapa nchini.

Amesema kuwa kupitia mpango huo uliozinduliwa wafugaji wanapaswa kuongeza mnyororo wa  thamani ya mifugo yao ili waweze kuzalisha kwa tija na kwa faida tofauti na walivyozoea kufuga kimazoea.

Aidha ameishukuru serikali  ya Beljam kwa kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 11 kuhakikisha mradi huo unatekelezeka katika wilaya za longido na simanjiro.

Nae mkurugenzi wa shirika la Trias  afrika mashariki bw Bart Casier  amesema kuwa wameamua kushirikiana na serikali ili kuwakwamua kiuchumi wafugaji katika kuhakikisha wanaondokana na changamoto zinazowakabili.

Amesema kuwa mbali na kusaidia miradi hiyo hadi sasa wamefainikiwa kusaidia vikundi vya vikoba 450  kwa kuwakopesha  pamoja na vyama vya kuweka na kukopa  (sacos) lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na sekta nyingine ili kukomboa jamii kwenye sekta za biashara,lishe,maji pamoja na mitaji.

Kwa  upande wake mkuu wa wikaya ya longido frenk Mwaisumbe amewashukuru maisha  bora  kwa kushirikiana na serikali kwa kuwawezesha mradi huo kwani anaamini utawanufaisha wafugaji lakini pia kuwanufaisha wanawake kwa kuwapatia mikopo.

Mwaisumbe alimalizia kwa kusema kuwa bado katika jamii   za wafugaji kunawanaofuga kama utamaduni hali ambayo inasababisha washindwe kufikia malengo yao lakini sasa kupitia mkakati  huo hali itabadilika

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post