Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetangaza ratiba ya uchaguzi wa viongozi wake ngazi ya Taifa.
Mchakato
huo unaanza na uchukuaji na urejeshaji fomu kuanzia Novemba 18 hadi
Novemba 30, 2019 huku mkutano mkuu ukifanyika Desemba 18, 2019.
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji akizungumza na wanahabari makao
makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam alisema uchaguzi
huo utaanza kwa kuchagua viongozi ngazi ya mabaraza na kufuatiwa na
viongozi wakuu wa chama ngazi ya Taifa.
"Tutakuwa
na Mkutano Mkuu wa Taifa itakuwa December 18, 2019, tushapeleka mialiko
kwa watu mbalimbali, miongoni mwa mambo tutakayoyafanya siku hiyo ni
kuchagua Viongozi Wakuu wa Chama
"Mchakato
tunaoanza nao ni kuchukua na kurudisha fomu za Wagombea, huu mchakato
unaanza November 18, 2019, wote ambao wangependa kugombea nafasi
mbalimbali wanakaribishwa kuja kuchukua fomu, kujaza kwa ufasaha na
kwenda kugombea" Amesema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji
Amesema
baada ya kupitia majina ya wote walioomba, Desemba 8, 2019 kamati
tendaji ya baraza la vijana na wazee watakutana na kufuatiwa na mkutano
mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa mabaraza hayo Desemba 9, 2019.
Dk
Mashinji amesema Desemba 10, 2019 kamati tendaji ya baraza la wazee na
vijana itakutana ambapo ni vikao vinavyofanyika kufuatiwa na mkutano
mkuu.
