Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa na
kauli za mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye aliyetangaza kukihama chama hicho.
Katika mkutano wake na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam uliofanyika leo, Sumaye ametangaza kujitoa
Chadema huku akitoa tuhuma mbalimbali kwa mwenyekiti wa chama hicho,
Freeman Mbowe.
Mkurugenzi
wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema
kuwa chama hicho hakikuwa na taarifa za mkutano huo uliofanyika leo na
kwamba wameona barua tu mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.
Mrema
amesema wamezipokea taarifa za Sumaye kuondoka Chadema na kama
mwanachama yoyote ameacha pengo kwenye chama hicho, kwamba watatafuta
namna ya kuziba pengo hilo.
“Hatuna
taarifa za makundi kwenye chama chetu kama anavyodai Sumaye, labda
kama yeye alikuwa na kundi. Sumaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya
chama alikuwa na nafasi ya kutoa taarifa hiyo na kama kweli ipo
ingefanyiwa kazi.
Kuhusu uchaguzi wa chama hicho
unaoendelea, Mrema amesema katiba ya Chadema hairuhusu mgombea kupita
bila kupingwa, kama mgombea ni mmoja lazima apigiwe kura ya ndio au
hapana.