Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla ameitaka Taasisi ya Utafiti
ya Wanyamapori Nchini{TAWIRI} kuwa na mpango kazi wa mnyama aina ya
Twiga katika hifadhi mbalimbali hapa nchini kwani kuna viashiria vya
wanyama hao kutoweka katika hifadhi za Taifa.
Dkt Kigwangalla ameyasema hayo
leo jijini Arusha,wakati akifungua kongamano la 12 lililoshirikisha
nchi 16 wana sayansi watafiti wa uhifadhi duniani,Wakurugenzi na
watendaji wa Taasisi za Uhifadhi nchini na mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali lililoandaliwa na Taasisi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania.
Amesema kuwa, katika mpango
kazi wao wa miaka mitano wa utafiti wa wanyama TAWIRI wanapaswa kuweka
mkazo wa kujuwa nini kinasababisha Twiga kutoweka katika hifadhi za
Taifa na kuja na majibu ya msingi juu ya hali hiyo ili serikali iweze
kutafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Waziri amesema Twiga ni nembo
ya Taifa hivyo ni wajibu wa watafiti wa taasisi ya TAWIRI kuhakikisha
wanapata majibu ya msingi kuhakikisha mnyama huyo hatoweki bali
anaongezeka katika mbunga za Taifa.
Amesema kuwa, utafiti mwingine
ambao TAWIRI inapaswa kuufanyia kazi ni pamoja na ndege wa Magharibi
mwa Tanzania na kusema kuwa ndege hao ni kivutio kikubwa katika kuvutia
watalii hapa nchini.
Dkt Kigwangalla amesema
kuwa,katika ukanda huo kuna ndege aina 700 hupatikana katika eneo hilo
la Magharibi mwa Tanzania hivyo ,Taasisi hiyo ya wanyama inapaswa
kufanyia kazi na kuyapeleka mapendekezo yake serikali.
Waziri ameagiza TAWIRI kuweka
nguvu zaidi kati suala la migogoro ya binadamu na wanyama kwani
changamoto hiyo imekuwa kubwa sana hapa nchini karibu hifadhi zote hapa
nchini hivyo lazima taasisi hiyo ifanye utafiti wa kina wenye lengo la
kupunguza ama kumaliza tatizo hilo.
Amesema utafiti huo unapaswa
kuja na jibu la msingi lenye tija kwa pande zote mbili ili mnyama awe
salama kwa faida ya uhufadhi na binadamu pia anapaswa kuwa salama na
kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Aidha Waziri aliitaka TAWIRI
walifanyie kazi swala la mito kwani wanyama aina ya Mamba na Kiboko
wamekuwa wakiwala binadamu mara kwa mara pindi binadamu anapokwenda
katika mito aidha kuchota maji ama kunywesha mifugo.
Amesema kuwa, tafiti zote
zikipelekwa serikalini na kufanyiwa kazi ana uhakika migogoro kati ya
binadamu na wanyama huenda ikaisha ama kupungua.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
TAWIRI,Dokta Saimon Mduma amesema kuwa, changamoto zote zilizosemwa na
Waziri asilimia kubwa zimeshaanza kufanyiwa kazi na mapendekezo yake
yatafikishwa serikalini kwa utekelezaji.
Dkt Mduma ametoa mfano wa eneo
ambalo tayari wameanza kulifanyia kazi ni pamoja na eneo la mito kwa
Mamba na kiboko kujengewa uzio ili binadamu wawe salama pindi
wanapokwenda katika mito kuchota maji ama kunywesha mifugo yao.
Amesema kuwa, kuhusu mgogoro
kati ya wanyama wakali kama tembo na simba kwenda katika maeneo ya raia
na kuua binadamu na mifugo , TAWIRI imeshaanza kulifanyia kazi na
watakuwa na majibu ya msingi nini kifanyike kwa serikali kumaliza
mgogoro huo.
Naye Mkurugenzi wa Utafiti wa
TAWIRI,Dkt Julius Keyyu amesema kuwa, katika utafiti wa Twiga duniani
imeonyesha kupungua kwa mnyama huyo katika hifadhi ,hivyo ni wajibu wao
hapa nchini kuhakikisha nembo hiyo ya Taifa inaongezeka katika mbugani
kutoka Twiga 29,000 kwa sensa ya mwaka 2016.
Dkt Keyyu amesema kuwa, sababu
kubwa inayochangia kwa asilimia kubwa Twiga kupungua katika hifadhi ni
pamoja na magonjwa mbali ya ngozi na masikio na wao wanajipanga
kuhakikisha tiba inapatikana ili suala hilo liweze kupotea kabisa.
Amesema kuwa,hivi sasa TAWIRI
imeweka mpango kazi wa miaka mitano wa kuhakikisha nembo hiyo ya Taifa
inaongezeka katika hifadhi mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na
kupambana na magonjwa wanayokutana nayo na kutoa elimu kwa jamii juu ya
uhifadhi wa Twiga na kumlinda mnyama huyo.