Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemuelekeza
Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Simon Sirro kuwaondoa Makamanda wa
Polisi wa Mikoa Miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba kwa
kushindwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 16 za Makazi ya Polisi
uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2018 na Makamu wa Rais,Samia Suluhu
Hassan pamoja na kuacha mikutano ya siasa ya Chama cha ACT Wazalendo
kuendelea Kisiwani Pemba hali ambayo kukaidi agizo la Kiongozi Mkuu wa
Nchi.
Masauni ametoa agizo hilo jana Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.
Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.
Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.