Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo pamoja na Makamanda wa Polisi pamoja na Kamati ya
Usalama Mkoa wakifurahia Wimbo ambao Askari wa Jeshi la Polisi walikua
wanaimba katika ufunguzi wa kikao kazi cha Makamanda wa Polisi Kanda ya
Kaskazini kilichofanyika katika bwalo la Maofisa wa Polisi Mapema leo
Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo (Katikati) akiwa amesimama pamoja na Makamanda wa
Polisi pamoja na Kamati ya Usalama Mkoa wakati wimbo wa Jeshi la Polisi
ukipigwa katika ufunguzi wa kikao kazi cha Makamanda wa Polisi Kanda ya
Kaskazini kilichofanyika katika bwalo la Maofisa wa Polisi Mapema leo
Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho gambo, Makamanda wa Polisi Kanda ya Kaskazini pamoja na
Kamati ya Usalama Mkoa wa Arusha katika ufunguzi wa kikao kazi cha
Makamanda wa Polisi kanda ya Kaskazini.
Maofisa na Askari wa
Vyeo mbalimbali wakifuatilia kwa makini Maelekezo mbalimbali yaliyokua
yanatolewa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Makamanda wa Polisi
Kanda ya Kaskazini kilichofanyika katika bwalo la Maofisa wa Polisi
Mapema leo Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na Makamanda wa Polisi Kanda ya Kaskazini pamoja na Maofisa, Wakaguzi na Askari wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Makamanda hao mapema leo Jijini Arusha. |
……………..
Na Gasto Kwirini wa Jeshi la Polisi Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo amewataka Makamanda wa Polisi Kanda ya Kaskazini
kuja na mikakati na mbinu za kisasa katika kukabiliana na matukio ya
uhalifu.
Ameyasema hayo wakati
akifungua Kikao kazi cha Makamanda wa Polisi kanda ya Kaskazini
ambacho kinahusisha Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi
Jijini Arusha.
Amesema pamoja na
Jeshi hilo kufanya kazi nzuri, amewataka Makamanda hao kujadili na
kuweka mikakati mipya na ya kisasa ambayo itawezesha katika kukabiliana
na matukio ya uhalifu na wahalifu hususani mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya, Uhalifu unaovuka mipaka, Ulinzi wa Madini na kuweka mazingira
mazuri ya kiusalama kwa sekta ya utalii.
‘‘Makamanda
shirikishaneni mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu, kwa sababu
Wahalifu hawatakuwa na sehemu ya kukimbilia kwa kuzingatia maeneo yote
katika kanda hii ya kaskazini mbinu za kihalifu zinafanana’’. Alisema
Gambo.
Naye Kamishna wa
Polisi Intelijensia ya Jinai CP. Charles Mkumbo ambaye pia ni Mlezi wa
Kanda hiyo amesema lengo la kikao kazi hicho ni kuweka mikakati ya
pamoja katika kuhakikisha Kanda hii inaendelea kuwa shwari hasa kwa
kuzingatia kanda hii ni kitovu cha utalii hapa nchini.
‘‘Nimekuja ili
kuhakikisha Makamanda hawa wanaungana pamoja, Kama ni msako ufanyike kwa
siku moja katika mikoa yote ili kuhakikisha wahalifu wanakosa sehemu ya
kujificha’’. Alisisitiza Kamishna Mkumbo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Makamanda wa Polisi Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga alisema wamekutana ikiwa ni utaratibu
wao wa kukutana kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kubadilishana
uzoefu wa kukabiliana na uhalifu.
Aliongeza kwa kusema
kuwa watajadili na kuweka mikakati ambayo watakuja na maazimio ya pamoja
ya kukabiliana na Matukio yote ya kihalifu hasa katika maeneo ya mipaka
ya Namanga, Holili, Hororo na Tarakea ili kuhakikisha Wahalifu wanakosa
sehemu ya kukimbilia.