Na Ahmed Mahmoud,Killimanjaro.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Same, Annaclair Shija amewasimamisha watumishi
wawili wa hospitali ya wilaya hiyo akiwemo Afisa Tabibu kwa kudai na
kupokea rushwa ya shs. 15,000/= kutoka kwa mama mwenye mtoto mchanga
mgonjwa wakike mwenye umri wa miezi mitano wa kijiji cha Vunta
kilichopo ukanda wa milimani mwa wilaya hiyo.
Shija amechukua
hatua hiyo baada ya afisa tabibu huyo Kimweri kihiyo amesimamishwa kwa
kumwandikia upasuaji mtoto huyo ambao hakustahili na kudai rushwa hiyo
huku mlinzi daniel kihara alimuuzia dawa kutoka bohari ya serikali
kwashs. 4,500/ kwa mama wa mtoto huyo ambaye alistahili apewe mtoto wa
miaka 12.
Aidha amesema,
vitendo vya aina hiyo vimekuwa vikiidhalilisha serikaliambayo imekuwa
ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia
90 na kitendo cha kumwandikia dawa na upasuaji ambao hakustahili ni sawa
mauaji .
Muuguzi wa
hospitali hiyo bw Fabian Bulili amesema kuwa afisa tabibu huyo ambaye
hakuwa kazini anaonyesha alikuwa na tabia ya kuwaandikia dawa wagonjwa
kwa ushirikiano na watumishi wasio waaminifu na kujipatia fedha
kuikosesha mapato halmashauri
Baadhi ya
wananchi wa wilaya hiyo eliabu mgonja wameipongeza hatua hiyo na
kueleza kuwa watumishi wa aina hiyo wanastahili kufukuzwa kazi ili
wananchi waendelee kupata huduma bora za afya bila kudaiwa rushwa.