Picha : RC TELACK AWAONYA WAFUNGWA WALIOPEWA MSAMAHA NA RAIS MAGUFULI




Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, amewaonya wafungwa ambao wamepewa msamaha wa kuachiwa huru na Rais John Magufuli kuwa wakajishughulishe kwenye shughuli halali za kuwaingizia kipato, kikiwamo kilimo, mifugo, pamoja na kufanya biashara mbalimbali na siyo kwenda kufanya uhalifu tena.

Telack ametoa onyo hilo leo, Desemba 10,2019 , wakati alipo kwenda Magereza kujiridhisha majina ya wafungwa 74 mkoani Shinyanga kama ni kweli wale ambao wamepewa msamaha na Rais Magufuli jana Jijini Mwanza, kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kati ya wafungwa 5,533 waliosamehewa nchi nzima.

Amesema kutokana na kipindi hiki ni cha msimu wa mvua, wafungwa hao 74 ambao wameachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli mkoani Shinyanga, wanatakiwa wakajikite kwenye shughuli za kilimo, mifugo, na kufanya biashara za kuwaingizia kipato halali, na siyo kurudi kwenye uhalifu.

“Natoa tahadhari kwenu nyie wafungwa ambao mmeachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli, msirudi uraiani kwenda kufanya matukio ya uhalifu tena, na bahati nzuri mmeachiwa kwenye kipindi kizuri cha msimu wa mvua, hivyo muende mkajishughulishe na kilimo ili mpate mavuno na kuinuka kiuchumi,” amesema Telack.

Naye Mkuu wa Magereza mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Magereza Dk.t Wilison Rugamba, amesema wafungwa ambao wameachiwa huru mkoani humo ni wale ambao waliobakiza vifungo vyao kuanzia siku moja, miezi sita, hadi mwaka mmoja, ambapo mkoani humo wameachiwa wafungwa 74, wa kiume 62 na wanawake 12.

Nao baadhi ya wafungwa hao akiwemo Bakari Juma mkazi wa Shinyanga, wamemshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa msamaha huo, huku wamkimuahidi mkuu huyo wa mkoa kutokwenda kufanya uhalifu tena, ikiwa baadhi yao wameshajifunza jinsi ya kilimo bora wakiwa magereza na wataenda kuendelea ujuzi huo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, akizungumza na wafungwa walioachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli kwenye Gereza la Shinyanga na kuwaonya wasirudie kufanya uhalifu bali wakajikite kufanya shughuli halali za kuwaingizia kipato. Picha na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mkuu wa Magereza mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Magereza Dkt Wilison Rugamba, akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa, kuwa wafungwa 74 wameachiwa huru mkoani Shinyanga, wanaume 62, wanawake 12.

Mfungwa aliyeachiwa huru kwenye Gereza la Shinyanga Revocatus Medard, kwa msamaha wa Rais John Magufuli, akishukuru kwa msamaha huo na kuahidi kutofanya uhalifu tena.

Mfungwa aliyeachiwa huru mkoani Shinyanga Bakari Juma kwa msamaha wa Rais John Magufuli, akishukuru kwa msamaha huo na kuahidi kutofanya uharifu tena, ambapo kwa sasa imebidi aokoke kabisa wakati akiwa humo Gerezani, na kuahidi kwenda kufanya shughuli za kilimo, ikiwa ujuzi wa kulima kitaalamu ameupata Gerezani.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post