Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Mohammed Kahundi (mwenye suti nyeusi) akizindua zoezi la
Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa
Shinyanga kwa kupulizia dawa ya viua dudu katika bwawa la Shunu lililopo
katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji leo Jumamosi Desemba
21,2019. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Mohammed Kahundi (mwenye suti nyeusi) akiendesha zoezi la
Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika bwawa la Shunu lililopo
katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi (katikati) akichota
maji katika bwawa la Shunu lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya
Kahama Mji ili kuangalia aina na idadi ya viluilui vilivyopo kwenye
bwawa la maji.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi na wadau mbalimbali wa
afya wakiwa katika bwawa la Shunu wakati wa kuzindua zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga.
Awali Afisa Afya halmashauri ya Ushetu Genoveva Gabriel akitoa ufafanuzi namna ya kuendesha zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu.
Mhudumu wa afya ngazi ya jamii kutoka kata ya Ulewe,Brown Christian akiendelea na zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika bwawa la Shunu.
Kulia ni Meneja Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC, Hamid Al- Alawy akimweleza jambo Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi wakati wa uzinduzi
wa zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu
mkoa wa Shinyanga kwa kupulizia dawa ya viua dudu katika bwawa la Shunu
lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.Wa kwanza kushoto
ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa Shinyanga.
Awali
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akizungumza na
watoa huduma za afya ngazi ya jamii na wadau wa afya katika Ukumbi wa
Kahama Super Logde Mjini Kahama. Kahundi alisisitiza elimu kuhusu
udhibiti wa ugonjwa wa malaria iendelee kutolewa kwa njia mbalimbali
zikiwemo wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii, Vituo vya afya, katika kaya na
kwa njia ya vyombo vya habari.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi akielezea mikakati
inayotumika mkoani Shinyanga kutokomeza malaria kuwa ni Upuliziaji wa
Viua Dudu katika mazalia ya mbu,upatikanaji wa vyandarua kwa wajawazito
na watoto wanaopata chanjo ya surua / rubella, upatikanaji wa dawa ya SP
kwa wajawazito kliniki, vyandarua shuleni, upimaji wa vimelea vya
malaria kwa wanaohisi kuwa na homa kwa kutumnia mRDT`s na upatikanaji wa
dawa mseto ya malaria.
Meneja
Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC,
Hamid Al- Alawy akielezea namna wanavyoshirikiana na serikali ya mkoa wa
Shinyanga katika kupambana na malaria.
Meneja
Mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC
Tanzania, Hamid Al- Alawy alisema asasi yake itatoa dawa na vifaa
kusaidia kufanikisha zoezi la upuliziaji wa viua dudu katika mazalia ya
mbu kwenye halmashauri ya Ushetu.
Mganga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akiipongeza na kuishukuru
asasi ya T MARC Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika
mapambano dhidi ya malaria na kuwaomba kutekeleza mradi wa Badilisha Tabia Tokomeza Malaria katika halmashauri ya Shinyanga ambayo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria baada ya Ushetu.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa
Shinyanga, Dkt. Daniel Mzee akitoa taarifa ya hali ya malaria katika
mkoa wa Shinyanga. Alisema vyandarua vyenye viuatilifu vinapatikana
katika vituo vyote kwa akina mama wajawazito wanaohudhuria kliniki kwa
mara ya kwanza na watoto wanaopata chanjo ya kwanza ya surua-rubella.
Wakurugenzi wa halmashauri
za wilaya,wajumbe wa timu ya usimamizi za afya mkoa na halmashauri,wadau
wa maendeleo na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakiwa ukumbini.
Mtoa huduma za afya Shema
Lupiga akielezea namna walivyonufaika na mafunzo kwa nadharia na vitendo
kuhusu namna ya kuendesha zoezi Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia
ya mbu.
Wakurugenzi
wa halmashauri za wilaya,wajumbe wa timu ya usimamizi za afya mkoa na
halmashauri,wadau wa maendeleo na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakiwa
ukumbini.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela akizungumza ukumbini.
Wajumbe wa timu ya usimamizi
za afya mkoa na halmashauri, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wadau
mbalimbali wa afya wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya waliopata mafunzo kuhusu namna ya kuendesha zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
……………………………………………..
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mohammed Kahundi amezindua zoezi la
Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’ katika mazalia ya mbu mkoa wa
Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kupambana na ugonjwa wa malaria
nchini ili kutekeleza kauli mbiu ya ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’.
Uzinduzi
huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 21,2019 katika bwawa la Shunu
lililopo katika halmashauri ya Mji Kahama na kuhudhuriwa na Wakurugenzi
wa halmashauri za wilaya,wajumbe wa timu ya usimamizi za afya mkoa na
halmashauri,wadau wa maendeleo asasi ya T- MARC Tanzania na wahudumu wa
afya ngazi ya jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu ulioongozwa na kauli mbiu ya ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’
Kahundi alisema Viuadudu vinavyotumika kuweka katika madimbwi ya maji
havina madhara kwa watu na mifugo hivyo kuwataka wananchi wasiwe na
wasiwasi pale wanapoona wataalamu wa afya wakiweka viuadudu hivyo kwenye
madimbwi na mabwawa.
“Ushiriki wa jamii ni nguzo
muhimu katika kutokomeza malaria.Ili kufanikisha zoezi la upuliziaji wa
viuadudu ni lazima jamii ishirikishwe ili kuepuka mitazamo hasi kuhusu
zoezi hili. Shirikisheni Viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na
kata,viongozi wa mila na dini na vikundi vya ngoma vinavyokubalika ili
kutokomeza malaria”,alisema Kahundi.
Kahundi alisema Maambukizi ya
ugonjwa wa malaria katika Mkoa wa Shinyanga ni asilimia 6.1 na kitaifa
ni asilimia 7.3 huku halmashauri ya wilaya ya Ushetu ikiongoza kwa
kiwango cha asilimia 11.1% katika mkoa wa Shinyanga.
“Hali ya kiwango cha
maambukizi ya malaria katika mkoa katika halmashauri ya Ushetu ni 11.1%,
Shinyanga 6.9%,Msalala 6.2%,Kahama Mji 3.7%, Manispaa ya Shinyanga 3.1%
na Kishapu 2.9%”,alisema Kahundi.
“Ugonjwa wa Malaria umekuwa
ni ugonjwa uliozoeleka, wananchi wamesahau kwamba ugonjwa wa malaria
unaua sana kwa muda mfupi mara tu usipopata matibabu kwa haraka, Malaria
hupunguza nguvu kazi, kupoteza rasilimali, mahudhurio hafifu mashuleni,
kupoteza maisha kwa wajawazito na kuharibika kwa mimba au kujifungua
kabla ya wakati”,alieleza Kahundi.
Alisema mkoa wa Shinyanga
unaendelea kupambana na ugonjwa wa malaria kwa njia mbalimbali ikwemo
kuharibu mazalio ya mbu, kutumia vyanadarua vyenye viuatilifu kuwapa
elimu wananchi elimu kuhusu malaria.
Akitoa taarifa ya hali ya
Malaria katika mkoa wa Shinyanga, Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga,
Dkt. Daniel Mzee alisema lengo la zoezi la Upuliziaji wa Viua Dudu ‘Larviciding’
katika mazalia ya mbu ni kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu moja ya
mikakati ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini ili kutekeleza kauli
mbiu ya ‘Ziro Malaria inaanza na mimi’
Dkt. Mzee alisema jumla ya
wahudumu wa afya 35 kutoka kata zote za halmashauri ya Ushetu wamepatiwa
mafunzo ya namna ya kupulizia viua dudu kwa ufadhili wa asasi ya T-
MARC Tanzania wanaotekeleza mradi wa ‘Badilisha Tabia Tokomeza Malaria’
kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupambana na ugonjwa wa malaria katika
halmashauri za wilaya za Ushetu, Msalala na Kishapu.
Alieleza kuwa maambukizi ya
malaria yanatokana na wananchi wengi kutotumia vyandarua vyenye
viuatilifu,elimu duni kuhusu malaria,usafi wa mazingira na imani potofu
juu ya matumizi ya vyandarua.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume aliwakumbusha wakurugenzi wa
halmashauri za wilaya kutenga fedha za kutosha katika mipango ya
halmashauri za kununulia dawa za viua dudu ili zoezi la kupulizia viua
dudu liwe endelevu katika halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga.
Naye Meneja Mradi wa Badilisha
Tabia Tokomeza Malaria kutoka asasi ya T- MARC Tanzania, Hamid Al- Alawy
aliiomba serikali kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliopatiwa
mafunzo na T -MARC Tanzania ili hata watakapomaliza kutekeleza mradi
wao wa ‘Badilisha Tabia Tokomeza Malaria’ kazi ya kupambana na malaria iwe endelevu.
“Wahudumu hawa wa afya
tumewapa ujuzi na utaalamu wa kutosha.T MARC inaahidi kutoa dawa na
vifaa vya kuanzia katika zoezi la upuliziaji viua dudu katika
halmashauri ya Ushetu”,alisema Alawy.
Mmoja wa watoa huduma za afya
waliopata mafunzo hayo, Shema Lupiga alisema mafunzo hayo yalifanyika
kwa nadharia na vitendo kuanzia Desemba 18 hadi Desemba 21,2019 kuhusu
namna ya kuendesha zoezi Upuliziaji wa Viua Dudu katika mazalia ya mbu.
Aliyataja baadhi ya maeneo ya mazalia ya mbu ‘viluilui vya mbu’ kuwa ni mashamba ya mpunga,mabwawa,mashimo ya choo,makopo na madimbwi.