Mkurugenzi
wa TAEC Profesa Lazaro Busagala Akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo
ya siku tano ya Uthibiti Usalama wa Mionzi katika Idara ya Radiolojia
nchini yaliyofanyika katika Kituo cha nguvu ya Atomiki jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wa mafunzonhayo ya siku tano wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika KituoKituo cha nguvu ya Atomiki jijini Arusha
Profesa Busagala akisisitiza jambo katika mafunzo hayo ya siku tano yaliyofanyika TAEC Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mafunzonhayo ya siku tano wakiwa katika ukumbi wa mkutano katika KituoKituo cha nguvu ya Atomik jijini Arusha
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo hayo Uthibiti Usalama wa Mionzi katika idara ya
radiolojia nchini yaliyofanyika katika Kituo cha nguvu ya Atomik
jijini Arusha.
Na.Vero Ignatus.
Jumla
ya hospitali 94 ambazo zinatoa huduma za Mionzi nchini zimefungiwa
kutokana na kutokidhi ubora wa utoaji huduma hiyo hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa kufunga Mafunzo ya siku tano ya Uthibiti Usalama wa Mionzi
katika idara ya radiolojia nchini yaliyofanyika katika Kituo cha
nguvu ya Atomik jijini Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho Profesa Lazaro Busagala alisema jumla ya hospitali zilizofanyiwa Ukaguzi ni 664 ambapo hospitali 105 zilifungiwa kutokana na kutokukidhi vigezo vilivyopo.
Profesa
alisema kuwa mara baada ya ukaguzi Hospitali kumi tu zilifunguliwa
kutokana na kukidhi vigezo na kufunguliwa ambapo mpaka sasa 95 bado
zimefunga kwa mujibu wa kaguzi za mwaka 2019/2020.
Aidha
aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanatumia vyema
taaluma zao katika kuhakikisha kuwa watanzania haawaathiriki na Mionzi
na pindi ambapo wanaona kuna changamoto katika maeneo yao ya kazi basi
waweze kuhakikisha kuwa wanashauri kwa kutumia maandishi na sio maneno.
“Tutachukua
hatua kali kwa wakuu wa hospitali ambazo hazitafuata taratibu
tutafungia moja baada ya nyingine mpaka taratibu zitakapofuatwa ili
watanzania waweze kuwa salama”alisema Profesa Busagala
Kwa
Upande wake Mkurugenzi Uthibiti na Usimamizi na Matumizi Salama ya
Mionzi Dkt.Justine Ngaile alisema kuwa baadhi ya mapungufu ambayo
yanapelekea hospitali hizo kufungwa ni pamoja na kukosa mtaalamu ambaye
ana ubora wa kutoa huduma hizo lakini pia Ubora wa mashine ambazo
zinatumika kwenye huduma ya mionzi kutokuwa na ubora ikiwa ni pamoja na
Jengo linalohidhi mionzi kutokuwa na ubora wa kutosha.
Hata
hivyo dkt.Ngaile alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa mionzi
hatarishi haiwezi kuwafikia wataanzania na kuwaletea Athari bali wawe
katika mikoni salama na kuhakikisha kuwa wataalamu wanaongezewa ujuzi
kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa teknolojia na Ufundi Filmi Banzi alisema kuwa
Tanzania ipo salama kwa kuwa tume ya nguvu za atomic ina ofisi zipatazo
26 mipakani kwa nchi nzima ili kuzui vyanzo holela vya Mionzi ambavyo
havihitajikikwa kutumia vifaa maalum ambavyo ni gunduzi kwa mionzi isiyo
salama.
Faustine
Mulyutu ambaye ni katibu wa wataalamu Mionzi Mikoa ya Tanzania Bara
aliiomba serikali kuhakikisha kuwa sekta ya wataalamu wa picha za mionzi
inapewa kipaumbele kama nyinginezo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi
uliotukuka.
Jumla
ya wataalamu wapatao 104 wamehudhuria mafunzo hayo wakiwa ni pamoja na
mariadiojia,madaktari,na wauguzi ambao wanahusikaa na namna moja ama
nyingine na mionzi ya mahospitaline.