Mkuu
wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akizungumza na wananchi
waliojitokeza katika stendi ya hiace Kilombero Jijini Arusha,kulia kwake
ni mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum,katika kampeni ya
usajili wa laini za simu kwa mfumo wa vidole iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akimpa maelekezo Afisa wa NIDA
Juliety Robert juu ya kuweka dawati kwaajili ya kuwasaidia wananchi
ambao wanamalalamiko .
Mkuu
wa kandaya kaskazini TCRA Mhandis Imelda Salum (Mwenye tisheti
nyeupe),kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro,wa
kwanza kushoto ni Afisa NIDA mkoa wa Arusha Juliety Robert ,wa kwanza
kushoto ni Katibu Tarafa wa Themi Felisian Gasper Mtahengelwa .
Afisa
wa NIDA mkoa wa Arusha akitoa ufafanuzi wa Jambo kwa mkuuu wa wilaya
Gabriel Daqqaro,kushoto kwake ni mkuu wa kanda ya Kaskazini TCRA imelda
Salum.
Mkutano ukiendelea katika stendi ya hiace kilombero.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya Stendi ya Haice ya Kilombero wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Arusha.
Kutoka
kushoto ni mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum akiwa
pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro katika stendi ya
Hiace Kilombero
Afisa
wa NIDA mkoa wa Arusha Juliety Robert akitoa ufafanuzi kwa wananchi
mara baada ya kutoa malalamiko kwa.mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel
Daqqaro kwamba wengine waneandikishwa zaidi ya mara tatu.
mkuuu
wa wilaya ya Arusha akisalimiana nawananchi katika tamasha la
kuhamasisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika stendi
ya hiace kilombero Jijini Arusha jana.
Wananchi
waliojitokeza kufuata namba zaonkatika stendi ya Hiace Kilombero Mkoani
Arusha kwenue Kampeni ya Usajilinwa simu kwaalama za vidole
iliyoandaliwa na TCRA kanda ya Kaskazini.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akiwa amewasili katika stendi ya
Hiace Kilombero katika kampeni ya kusajili laininza simu kwa mfumo wa
alama za vidoleniliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akisalimiana na wananchi
waliojitokeza katika stendi ya Kilombero Jijini Arusha wengi wao wakiwa
ni wafanya biashara .
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akijisajili kwa alama ya Vidole
kwenye kampuni ya simu TTCL tayari katika viwanja vya Stendi ya haice
Kilombero Jijini Arusha.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akijisajili kwa alama ya Vidole
kwenye kampuni ya simu TTCL tayari katika viwanja vya Stendi ya hiace
Kilombero Jijini Arusha.
Na.Vero Ignatus,Arusha
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Kanda ya Kaskazini imewataka wananchi imewataka watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchukua tahadhari dhidhi ya utapeli kwenye mitandao ya simu za mkononi wala kutekeleza maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa maandishi hata kama yanatoka kwa namba ya mtu wanaomfahamu.
Akitolea ufafanuzi juu ya jambo hilo jana, Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum katika tamasha la uhamasishaji wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole Jijini Arusha ,amesema Sheria inamtaka mtumiaji au anayenunua laini ya simu kuisajili majina halisi kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na posta (EPOCA) amewataka taarifa wanazozitoa wakati wa kusajili laini za simu ziwe za kweli kwani ni kosa la jinai kutoa taarifa ambazo siyo sahihi.
''Ikithibitishwa Mahakamani kuwa umetoa taarifa za uongo,adhabu kali hutolewa ikiwa ni pamoja na faini kifungo au vyote viwili,sajilini laini zenu za simu kwa usahihi kabla ya muda uliowekwa wa desemba 31 kumalizika''alisema
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ameiomba Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kuongeza uhamasishaji wa watu kusajili laini za simu zao, hadi siku za Jumapili, ili kufikia laini milioni 47
zilizolengwa kusajiliwa.
Daqqaro alisema,hadi sasa laini zilizosajiliwa ni milioni 19 nchi nzima, idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na idadi iliyotarajiwa milioni 47 hivyo amewataka wananchi wa Jiji la Arusha ifikapo desemba 31 mwaka huu kila mmoja awe ameshasajili laini yake ya simu ya mkononi.
“Kutokana na idadi ya waliojiandikisha kuwa ndogo, natoa hamasa kwa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuongeza juhudi na
kufanyakazi hadi siku ya Jumapili kuandikisha watu ili kuwafikia
wananchi,”alisema.
Daqqaro alisema zoezi hilo la usajili linatambulika kisheria na kiutaratibu,hivyo uwepo wa usajili kwa njia ya alama za vidole gumba,itasaidia kuwa na kanzi data yakujua takwimu za watumiaji wa mitandao
ya simu kila mikoa na kupunguza wimbi la utapeli na uhalifu wa
mitandao na kuimarisha usalama.
"Zoezi hili ni zoezi nyeti sana na mtu anapofanya usajili wa laini
yake analazimika kutumia kidole chake, ili kupata taarifa muhimu na
pale anapofanya uhalifu atajulikana, hivyo kwakiasi itapunguza
uhalifu,”alisema.
Aidha alisema katika uzinduzi huo ananchi wengi amejitokeza kusajili
laini zao, lakini changamoto inayojitokeza baadhi ya wananchi
kutokuwa na vitambulisho vya Nida.
“Lakini sisi kama serikali naahidi tutaongeza mashine ili kuondoa
msongamani huu ninaouona wa wananchi ilia pate huduma ka haraka na
kwenda kuendelea na shughuli za uzalishaji mali,”alisema.
Aliataka makampuni ya simu yanayotoa huduma katika viwanja hivyo vya
standi ya daladala kuhakikisha yanasogeza huduma kwenye maeneo ya
soko na mikusanyiko ya watu ili kuwafikia walio wengi.
Awali baadhi ya wananchi waliohudhuria kampeni hiyo, Huruma Juma na
Sophia Ismail waliomba NIDA kupunguza urasimu eneo la Kisongo na
kufanya kazi siku za Jumapili, ili kuondoa msongamano wa wananchi
anaojitokeza kusajili laini zao.
Kampeni hizo za usajili wa laini za simu zinaishia Desemba 31 mwaka
huu na zinaratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye
kauli mbiu "Aachwi mtu nyuma, kamilisha usajili".