Kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Jonathan Shanna akionyesha moja ya silaha waliyokutwa nayo majambazi hao
silaha mbalimbali na simu za mkononi walizokutwa nazo majambazi hao baada ya kuuawa wakati wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu
Mkuu wa mkoa wa
Arusha ,Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya
jeshi la polisi kufanikiwa kuwaua majambazi watano mkoani Arusha
……………………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, APC BLOG, ARUSHA
WATU watano wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi, wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa baada ya kutakiwa kujisalimisha na kukaidi amri hiyo na kisha kuanza kuwarushia risasi askari.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani
Arusha,Kamanda wa polisi Jonathan Shanna amesema kuwa,tukio Hilo
limetokea januari 29 mwaka huu majira ya saa 3:45 asubuhi katika njia
panda iliyoko eneo la Mateves kata ya Olmot Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kamanda Sabas amesema
kuwa,tukio hili limetokea baada ya jeshi la polisi kupata taarifa fiche
kuwa majambazi hao walikuwa wamepanga kwenda kufanya tukio la ujambazi
katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Alisema
kuwa,majambazi hayo walipanga kutumia barabara ya Afrika Mashariki
(Bypass) kupitia Olasiti Hadi mzunguko wa kwa mrombo kwa kutumia usafiri
wa pikipiki tatu ambazo walikuwa nazo .
Amesema kuwa,Mara
baada ya polisi kupata taarifa hizo waliweka mtego katika njia panda ya
Mateves ambapo ilipofika majira ya saa 3:45 usiku Askari hao walionao
pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatokea upande wa Mateves kuelekea
barabara mpya ya Afrika Mashariki ,ambapo walisimamishwa na Askari hao
lakini badala ya kutii amri majambazi hayo walianza kufyetua risasi.
Ameongeza kuwa,baada
ya kukaidi amri hiyo ndipo kikosi cha askari waliokuwa wakiwawinda majambazi hao kilianza kujibu mapigo ambapo majibizano hayo
yalichukua muda takriban dakika 35 , ambapo majambazi wanne walifariki
hapohapo huku jambazi mwingine Mmoja aliyekuwa nyuma aligeuza na
pikipiki yake na kukimbia umbali was mita 500 lakini naye alipigwa
risasi na kudondoka.
Aidha katika eneo la
tukio walikuta vitu mbalimbali vilivyokuwa vinatumiwa na majambazi hao
ikiwemo pikipiki tatu ambazo ni MC 871 BWR aina ya Skygo ,MC 555 CGE
aina ya Kinglion ,MC 478 AYV aina ya Toyo,bunduki moja aina ya Shortgun
pump action yenye namba 32265,Chinese Pistol moja iliyofutwa namba zake
za usajili ,bastola moja ya bandia.
Amevaja vitu vingine
kuwa ni magazine mbili za Chinese ,Pistol moja ikiwa na risasi 8 na
nyingine ikiwa na risasi 1 .maganda 7 ya risasi ya Chinese Pistol,risasi
2 za bunduki aina ya Shortgun,maganda 5 ya risasi ya Shortgun na simu
mbili aina ya Tecno na moja aina ya Oking.
Aidha amesema kuwa,
uchunguzi wa awali umebaini kuwa bunduki hiyo aina ya Shortgun pump
Action iliibiwa januari 26,mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku nyumbani
kwa Jackson Msangi baada ya majambazi hao kuvunja nyumba yake iliyopo
maeneo ya Burka kata ya Olasiti.
Amesema
kuwa walifanikiwa pia kuiba simu ya mkewe aitwaye Nikira Msangi ambapo
yeyena mume wake wametambua bunduki na simu vilivyoibiwa siku hiyo
waliyovamiwa.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount meru kwa uchunguzi wa Daktari na utambuzi.
“Tunatoa onyo Kali
kwa watu wote wenye tabia ya kuvuna bila kupanda kuacha tabia hiyo mara
moja kwqni hatutasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria ,na tunatoa
rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa
taarifa za kihalifu ili tuweze kutokomeza kundi la watu wachache
wanaochafua mkoa wetu”amesema Kamanda Shanna.
Mkuu wa mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha amelipongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri waliyoifanya
ya kuwaua majambazi hao kwani wangeweza kusababisha madhara makubwa
huko walipopangiwa kwenda kufanya uhalifu.
Gambo amesema
kuwa,usalama ni kipaumbele chetu na mkoa wa Arusha ni mkoa wa kitalii
kwani asilimia 25 ya fedha zinazopatikana zinatokana na utalii,hivyo
kuna haja kubwa ya kuimarisha ulinzi kuhakikisha watalii wanakuwa salama
muda wote.